Zimesalia siku tisa tu kuanza kwa ligi kuu soka England (EPL) msimu wa 2015/2016 na timu zote zipo hatua ya mwisho ya maandalizi.
Manchester United wataanza kurusha karata ya kwanza dhidi ya Tottenham Agosti 8 mwaka huu.

David De Gea amekuwa akihusishwa sana kuhamia Real Madrid, ingawa United wanabania dili hili.
Alfajiri ya leo, Mashetani wekundu wamefungwa magoli 2-0 na miamba ya Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG) katika mechi ya mwisho ya International Champions Cup kujiandaa na msimu mpya iliyopigwa mjini Chicago, Marekani.
De Gea amecheza chini ya kiwango na kocha wa Man United, Louis van Gaal alimtoa baada ya dakika 45 za kipindi cha kwanza.
Kutokana na hali hii, Van Gaal sasa anawaza mawili, amruhusu aende Real Madrid au ampe mkataba mwingine, lakini ajue kwamba ana golikipa ambaye anaonekana kukosa 'focus' na timu kwasasa.

Magoli ya PSG yamefungwa na Blaise Matuidi dakika ya 25 na Zlatan Ibrahimovic dakika ya 34.