Wachezaji wa Azam wakisherekea ushindi baada kuilaza Yanga kwenye mhezo wa robo fainali uliochezwa jana kwenye uwanja wa Taifa
Golikipa wa Azam FC Aishi Manula akifanyiwa mahojiano na kituo cha Super Sport baada ya kumalizika kwa mchezo wa robo fainali kati ya Azam na Yanga ambapo alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo
John Bocco akimnyanyua juujuu Agrey Morris baada ya kupiga na kufunga penati ya mwisho ilioipa ushindi Azam FC na kusonga mbele kwa hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Kagame
Shabiki wa maarufu wa Azam FC anaefahamika kwa jina la Stive ambae alihama kutoka Yanga akiwakejeli mashabiki wa Yanga kwa kuwazomea baada ya timu yake kuishinda Yanga kwenye changamoto za penati na kusonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali
Shabiki maarufu wa Yanga Ally Yanga akiwa haamini matokeo ya mchezo wa robo fainali baada ya timu anayoishangilia kuenguliwa kwenye michuano ya Kagame katika hatua ya robo fainali
Mchezaji wa Azam FC Shah Farid Mussa (kulia) akijaribu kumtoka mlinzi wa kumtoka mlinzi wa Yanga Joseph Zutah
Winga wa Yanga Godfrey Mwashiuya akiruka kwanja la beki wa Azam FC Agrey Morris wakati wa mchezo wao wa robofainali