Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

SUB YA JOHN TERRY YAWAGAWA WACHAMBUZI, WEWE UNASEMAJE?

$
0
0
Graeme Souness amepinga mawazo ya mchambuzi mwenzake wa soka anayedai kwamba kitendo cha John Terry kutolewa jana katika mechi dhidi ya Manchester City ni kumtaarifa mmiliki wa klabu hiyo, Roman Abromavic kuwa maisha ya soka ya nahodha huyo yanaelekea ukingoni.
Kwa mara ya kwanza nafasi ya Terry ilichukuliwa na Kurt Zouma baada ya dakika 45 tu.
Haijawahi kutokea Kwa Terry kufanyiwa 'sub' katika mechi 177 chini ya kocha Jose Mourinho.
It was the first time in the Premier League under his current manager that the defender had been hauled off
Akizungumza kwenye uchambuzi wa baada ya mechi wa Sky Sports, Souness, anaamini Terry alitolewa kwasababu tu ya presha ya Mourinho.
"Nadhani Terry alikuwa bora kuliko Gary Cahill, sikuona kama alicheza vibaya. John Terry ni kiongozi". Alisema Souness.
Graeme Souness believes Terry's substitution was down to Mourinho's frustrations in the transfer market
"Nadhani kocha anajaribu kumwambia kwa vitendo mmiliki wa timu kwamba anahitaji wachezaji zaidi. Kama stori ni za kweli basi anapenda wachezaji wengi (Mourinho). Nadhani alikuwa anasisitiza hoja hiyo kwa vitendo akimtoa Terry".

Souness alikuwa anabadilishana mawazo na mchambuzi mwenzake, Niall Quinn, ambaye alidai kwamba kitendo hicho ni dalili ya soka la nyota huyo wa zamani wa England kumalizika.
Quinn, mchezaji wa zamani wa Manchester City anaamini sasa Terry anakabiliwa na changamoto ya kupigania namba yake katika kikosi cha kwanza.
Terry looked understandably disappointed on the substitutes bench during the Manchester City match 
"Tuliona picha zake akiwa kwenye benchi baada ya sub, naamini yeye mwenyewe ameshaanza kuwaza kwamba anakwenda kugombania namba kwenye timu".
"Sidhani kama Terry atacheza wikiendi ijayo (dhidi ya West Brom). Naamini ana kazi kubwa ya kumshawishi kocha wake. Huu unaweza kuwa mwanzo wa kuisha kwa soka lake".

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles