Xherdan Shaqiri amejibu mapigo kwa Stefan Effenberg baada ya mchezaji huyo wa zamani wa Ujerumani kudai kuwa winga huyo ameshauriwa vibaya kujiunga na Stoke City.
Shaqiri mwenye asili ya Switzerland, amevunja rekodi ya usajili kwa klabu ya Stoke baada ya usajili wake kugharimu kitita cha pauni milioni 12 akitokea klabu ya Inter mwanzoni mwa wiki hii, uhamisho ambao, kutokana na Effenberg, amesema umechangiwa na uroho wa pesa.
Lakini Shaqiri, kwa upande wake, ambaye mchezo wake wa kwanza unaweza ukawa dhidi ya Tottenham siku ya Jumamosi, amesisitiza kwamba yeye hajali anachokisema kiungo huyo wa zamani wa Bayern Munich.
“Hana kazi ya kufanya kwa sasa, hivyo muache tu aongee– yuko huru kusema chochote”, alisema Shaqiri ambaye ana umri wa miaka (23) kwa sasa.
“Yeyote ambaye anataka kuzungumza, azungumze tu. Lakini mimi sitasema chochote.
“Kwa sasa naangalia ajira yangu mpya – nina furaha kubwa kuwa hapa, na nasubiri kwa hamu mchezo wangu wa kwanza. Hii ni kazi yangu. Sio kazi yangu kujibu wanachokisema watu”.