Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

VAN GAAL AMESEMA SABABU HIZI HAPA KWA NINI DE GEA HACHEZI KWA SASA

$
0
0
David de Gea, ambaye anawindwa vikali na klabu ya Real Madrid anaonekana kuwa katika hatua za mwisho kujiunga na miamba hiyo ya Uhispania, baada ya kocha wake Louis Van Gaal kufichua kuwa mlinda mlango huyo hataki kuitumikia klabu ya Man United, hali inayopelekea mustakabali wake kuwa haueleweki klabuni hapo.
Tetesi zilizopo zinadai kuwa kuanzia mwezi Julai Manchester United, tayari walikuwa wamejiandaa kisaikolojia kumpoteza golikipa huyo ambaye alianza kuonesha dalili zote za kujiunga na Madrid na hivyo kuukosa mchezo wa ufunguzi wa ligi, ambapo United walishinda kwa goli 1-0 dhidi ya Tottenham Hotspurs.
"Tuliongea naye [De Gea] na alikubaliana na maamuzi yetu", Van Gaal aliwaambia waandishi.
"Nina makocha wasaidizi wawili na niliwaambia hicho kitu pia. Tuna kocha wa makipa pia, hivyo sio kwamba mimi nafanya maamuzi peke yangu.
"Frans Hoek… ana kikao na David de Gea na alimuuliza kuhusu hilo, ' je, unataka kucheza?' [De Gea alijibu "hapana"]. Basi nikaamua kufanya maamuzi. Kwa hiyo huu ni mchakato.
"Tumekuwa tukimwangalia kwa makini sana wakati wa maandalizi, hakuwa sawa, hakuwa David de Gea ambaye sote tumekuwa tukimfahamu. Alikuwa ni mchezaji wangu bora msimu uliopita. Kulingana na mashabiki, alikuwa ni mchezaji bora wa klabu kwa mika miwil".

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles