Klabu ya ARSENAL imeanza vibaya msimu wa 2015/2016 wa ligi kuu ya ENGLAND baada ya kukubali kichapo cha magoli mawili kwa bila kutoka kwa WESTHAM UNITED katika mechi iliyopigwa uwanja wa EMIRATES.

Mabao ya Wagonga nyundo wa LONDON yamefungwa na CHEIKHOU KOUYATE dakika ya 43 na MAURO ZARATE dakika ya 57.
Kwingineko, NEWCASTLE UNITED imetoka sare ya magoli mawili kwa mawili dhidi ya SOUTHAMPTON.
PAPISS CISSE na GEORGINIO WIJNALDUM wameifungia NEWCASTLE, wakati GRAZIANO PELLE na SHANE LONGwamecheka na nyavu kwa upande wa SOUTHAMPTON.