Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

MALINZI ATOA KAULI KUHUSU AZAM FC KUTINGA NUSU FAINALI KAGAME

$
0
0
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi ametuma salamu za pongezi kwa klabu ya Azam FC kwa kufanikiwa kuingia katika hatua ya nusu fainali ya Kombe la Kagame. 
Katika salamu zake kwa uongozi wa klabu ya Azam, Malinzi amewataka kutobweteka na kuongeza bidii katika hatua hiyo ya nusu fainali ili waweze kufuzu kwa hatua ya fainali na kutwaa Ubingwa huo na kuwaomba watanzania wote kuwasapoti wawakilishi hao pekee wa nchi kwenye michuano hiyo
TFF kwa niaba ya familia ya mpira na watanzania wote, inatwakia kila la kheri Azam FC katika mchezo wake wa kesho wa nusu fainali dhidi ya KCCA.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles