Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambi rambi kwa familia ya Moshi Shaban, kufuatia kifo cha Moshi kilichotokea jana jijini Dar s salaam na mazishi kufanyika leo jijini Dar es salaam.

Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya marehemu Moshi, TFF imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wako pamoja katika kipindi hiki cha maombelezo na kuomba mwenyezi Mungu awajilie nguzu wafiwa
Marehemu Moshi Shaban ni baba wa wachezaji waliowahi kuichezea timu ya Taifa ya Tanzania, Haruna Moshi “Boban) na Iddy Moshi (Mnyamwezi).


