Hatimaye burudani ya ligi pendwa zaidi Duniani inakaribia kuanza, lakini swali kubwa linabaki: Chelsea wataweza kutetea ubingwa wao?
Klabu ya Arsenal, Manchester City, Manchester United na Liverpool zinaonekana kupania zaidi kusaka ndoo ya English Premier League msimu wa 2015/2016.
Man United itacheza na Tottenham siku ya ufunguzi Agosti 8 mwaka huu na tayari kocha wa klabu hiyo, Mholanzi, Louis van Gaal ameweka wazi baadhi ya mipango ya mechi hiyo.
Walinzi wa England, Chris Smalling na Phil Jones wanapigania nafasi moja katika kikosi cha Manchester United baada ya Van Gaal kuweka wazi kwamba,
Luke Shaw, Matteo Darmian na Daley Blind wataanza katika safu ya ulinzi dhidi ya Tottenham.
Blind amecheza nafasi ya mlinzi wa kati kushoto kwenye mechi zote za United ilizocheza katika ziara ya Marekani na mapema Alfajiri ya leo alianza katika kikosi kilichopigwa 2-0 na PSG katika uwanja wa Soldier Field, Chicago.

Van Gaal: "Natakiwa kuanza na mfumo niupendao (3-5-2) na mfumo unapofanya kazi nawaacha wacheze katika mfumo huo."
"Nadhani nitawachezesha Shaw, Blind na Matteo Darmian, nafasi ya mlinzi wa kati kulia nitaamua".
"Nimevutiwa na Darmian, kama mnavyoona, anaweza kucheza kushoto na kulia".
