Mathieu Flamini amemshukuru Jose Mourinho kwa kumuuza Petr Cech kwa Arsenal.
Cech alihitimisha uhamisho uliogharimu pauni milioni 11 kuelekea Emirates mwezi uliopita, na kukamilisha miaka yake nane aliyodumu na Chelsea.
Flamini amekiri kwamba alishutwa na maamuzi ya Mourinho kumruhusu Cech kuhama klabuni hapo , na anaamini kwamba maamuzi hayo bado yanaweza kumtafuna mwenyewe, huku Cech akitarajiwa kukutana na Mourinho katika mchezo wa ngao ya jamii utakaopigwa Jumapili.
“Nilishangazwa sana na Mourinho kwa sababu mara zote huwa hafanyi hivyo”, alikariririwa na Daily Telegraph.
"Ni mshindani na siku zote hapendi kuuza mchezaji kwa wapinzani wake, lakini ni nafasi nzuri kwetu na tunatakiwa kunufaika kwa hilo kwa bahati tuliyoipata.