Liverpool imeshinda mechi ya tatu mfululizo katika ziara yake Mashariki ya Mbali na Austaria baada ya kuichapa 2-0 Adelaide United katika mechi ya kirafiki iliyopigwa mchana huu ikiwa ni maandalizi ya msimu mpya.
Magoli ya Liverpool yamefungwa na James Milner na Danny Ings.
Ings amefunga goli lake la kwanza tangu ajiunge na Liverpool kutoka Burnley, wakati Milner amefunga la pili wakati huu wa maandalizi ya msimu mpya.

James Milner (kushoto) akimalizia krosi ya Jordon Ibe na kufunga goli la kuongoza kwa Liverpool

Jordan Ibe (kushoto) akimpongeza Milner (wa pili kulia) baada ya kufunga goli leo

Mashabiki 53,000 wametazama mechi hiyo..