Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

SCHWEINSTEIGER APAGAWA NA KINDA HUYU WA MAN UNITED

$
0
0
Bastian Schweinsteiger amemuelezea mchezaji mwenza wa Manchester United Memphis Depay kama "kipaji kisichoelezeka", baada ya kumuona katika mchezo wake wa kwanza kwenye mechi maandalizi ya msimu mpya wa ligi.
Kiungo huyo wa kimataifa wa Ujerumani, ambaye amesajiliwa kutoka Bayern Munich kwa kitita cha pauni milioni 14, aliingia kipindi cha pili katika mchezo dhidi ya Club America na kuisaidia timu yake kuibuka na ushindi wa goli 1-0 katika dimba la CenturyLink.
Akiongea na tovuti ya klabu baada ya ushindi huo, Mjerumani huyo amesema kuwa ana imani kubwa mashabiki wa klabu hiyo wafaidi makubwa kutoka kwa Depay.
"Memphis ni kipaji kisichoelezeka na ana ubora wa hali ya juu na nina uhakika tutafurahia sana atakachokuwa akikifanya uwanjani pindi msimu utakapoanza", alisema.
"Nimefurahi sana kwa sababu kuwaangalia vijana namna wanavyocheza kwa mfano [Andreas] Pereira, Jesse [Lingard] na [James] Wilson. Wote ni wachezaji wazuri.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles