
Anamaanisha hivi: "Nimepokea kwa masikitiko makubwa sana taarifa za kifo cha kipa wa timu yetu ya taifa ya Uganda Cranes Abel Dhaira kilichotokea nchini Iceland kutokana na ugonjwa wa kansa. Ni masikitiko makubwa sana ameondoka akiwa na umri mdogo, hata hivyo tunatambua mchango wake kwa taifa letu. Serikali itagharamia kila kitu katika kuhakikisha mwili wa marehemu unarudi salama. Mungu aipe nguvu familia na marafiki wa Dhaira katika kipindi hiki kigumu wanachopitia. Mungu ailaze roho yake mahali pema".
I have received the sad news of the passing of our Uganda Cranes goalkeeper Abel Dhaira who succumbed to cancer in...
Posted by Yoweri Kaguta Museveni on Monday, 28 March 2016