Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

AUBEMAYANG AJIBU MAPIGO KWA YAYA TOURE

$
0
0
Mshambulizi wa Borussia Dortmund Pierre-Emerick Aubameyang amesikitishwa na kauli ya Yaya Toure baada ya kukosa tuzo ya mchezaji bora Afrika.
Toure alidhani yeye ndiye angetangazwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mara nne mfululizo, lakini alipewa Aubameyang ambaye amekuwa na rekodi nzuri ya magoli kunako ligi ya Bundesliga.
Toure alimpongeza Aubameyang lakini aliuita upigaji kura ni wa kipuuzi na usio na heshima na umelitia aibu bara la Afrika, sababu ikiwa ni kuangalia mafanikio ya Aubameyang katika klabu kuliko mafanikio yake aliyopata na timu ya taifa Ivory Coast baada ya kuipa kombe la Mataifa ya Afrika.
Akijibu hoja hiyo, Aubameyang alisema: "Sijui kabisa ni kwa nini alisema vile aisee."
"Siwezi kukasirishwa na hali hiyo na kwangu mimi hiyo hayo ni mambo ya kale tayari. Kifupi ni kwamba sijapendezewa na hali hiyo."

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles