Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

BARCA WAINYUKA BETIS 4-0 NA KUVUNJA REKODI HII

$
0
0
Lionel Messi amefanikiwa kuifungia Barcelona goli katika mechi yake ya 500 kwa timu hiyo huku wakifanikwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0.
Messi alifunga goli hilo baada ya kupoke apasi murua kutoka kwa Neymar ambaye aliambaa kutoka pembezoni mwa uwanja.
Magoli mengine ya Barcelona yalifunga na Heiko Westermann ambaye ni beki wa Betis baada ya kujifunga katika harakati za kuokoa mpira baada ya Neymar kukosa penati, huku Luis Suarez akifunga mabao mawili katika dakika za 46 na 83 na kufanya Barca kufikisha magoli 180 kwa mwaka 2015, wakiivunja rekodi iliyowekwa na Ancelotti alipokuwa Real Madrid mwaka 2014 kwa magoli manne zaidi.
Goli la Messi ambalo alifunga dakika ya 33 linamfanya afikishe idadi ya magoli 425 katika michezo 500 aliyoichezea Barca.
Lionel Messi (kushoto) amefurahia sana mafanikio ya timu yake katika mwaka wa kalenda wa 2015
Messi akimtoka beki wa Real Betis
Kabla ya mchezo huo wachezaji wa Barcelona walikusanyika wakiwa na makombe matano waliyochukua mwaka 2015 kunako dimba lao la Nou Camp
Barca mwaka huu wameshinda makombe ya La Liga, Copa del Rey, Ligi ya Mabingwa, European Super Cup and the Club World Cup.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles