Wachezaji wa Barcelona wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Dunia kwa mara ya tatu baada ya kuwafunga River Plate ya Argentina kwa mabao 3-0
Neymar, Luis Suarez na Lionel Messi wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza lililofungwa na Messi.
Lionel Messi amerudi tena kwa kasi ya aina yake kutoka majeruhi na kufunga goli murua huku Barcelona ikiwatungua River Plate ya Argentina kwa 3-0 na kuchukua ubingwa wa Club World Cup kwa mara ya tatu.
Messi alifunga goli lake mnamo dakika ya 36, kabla ya Muruguay Luis Suarez kuongeza mengine miwili mnamo dakika za 49', 68' katika mchezo uliopigwa kunako huko Yokohama.