Bayern Munich wamethibitisha rasmi kwamba Carlo Ancelotti atachukua mikoba ya Pep Guardiola baada ya msimu huu wa ligi kumalizika.
Guardiola, amejipatia mafanikio makubwa akiwa na miamba hiyo ya Ujerumani, baada ya kushinda makombe mawili ya Bundesliga, moja la DFB-Pokal, Uefa Super Cup na Fifa Club World Cup, lakini ameamua kuondoka klabuni hapo baada ya kuamua kutoongeza mkataba.
Na Karl-Heinz Rummenigge amethibitisha kwamba Ancelotti, ambaye ambaye yuko mapumzikoni mara baada ya kufukuzwa na Real Madrid mwezi Mei, amethibitishwa kuchukua mikoba hiyo.
"Tunashukuru sana kwa kila kitu ambacho Pep Guardiola amefanya katika klabu hii tangu mwaka 2013. "Ninashwishika kusema kwamba Pep na timu yake sasa watafanya kazi kwa bidii zaidi ili kupata mafanikio zaidi kwa sababu ni wazi kuwa Pep ataondoka FC Bayern," alisema katika taarifa iliyotolewa na klabu.
"Carlo Ancelotti amepata mafanikio kila sehemu alipofanya kazi. Ameshinda kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya mara tatu. Carlo ni mkimya, mwenye weledi ambaye pia anaweza kuishi na mchezaji yeyote anayependa soka la aina yoyote. Tunategemea mazuri kutoka kwake. Tunasubiri kwa hamu kufanya nate kazi."