Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all 1447 articles
Browse latest View live

ORODHA YA MAKIPA SITA NGULI DUNIANI

$
0
0
6. Julio Cesar-InterMilan (Brazil)
Tuzo binafsi
Kipa bora wa Serie A mwaka, 2008–09, 2009–10
Kipa bora wa UEFA mwaka : 2009–10
Kipa bora wa kombe la shirikisho mwaka 2013: 
FIFA Confederations Cup Dream Team: 2013
Primeira Liga Best Goalkeeper: 2014–15

5. Peter Shilton-Nottingham Forest (England)
Tuzo binafsi.
Kipa bora wa ligi daraja la kwanza mwaka: 1974–75, 1977–78, 1978–79, 1979–80, 1980–81, 1981–82, 1982–83, 1983–84, 1984–85, 1985–86

Mchezaji bora wa wachezaji mwaka: 1977–78

Mchezaji bora wa Nottingham Forest F.C. mwaka: 1981–82

Mchezaji bora wa Southampton F.C mwaka: 1984–85, 1985–86


4. Petr Czech-Chelsea,Arsenal (Jamhuri ya Cech)
Tuzo binafsi

Mchezaji bora wa UEFA Europa chini ya miaka 21: 2002

Kipa bora wa Ligue 1: 2003–04

Timu bora ya mashindano ya UEFA Euro 2004 

Kipa bora wa EPL : 2004–05, 2009–10, 2013–14

Mchezaji bora wa EPL mwaka: 2004–05, 2013–14

Mchezaji bora wa Czech mwaka: 2005, 2008, 2009,2010, 2011, 2012, 2013

Mpira wa dhahabu (Jamhuri ya Czech) : 2005, 2006, 2007, 2008, 2010, 2011, 2012, 2013
Kipa bora wa dunia wa IFFHS: 2005
Kipa bora wa klabu katika michuano ya UEFA: 2005, 2007, 2008
Mchezaji bora wa wa mwezi wa Chama cha soka nchini Uingereza (FA) Premier League Player of the Month: March 2007
Mchezaji bora wa mwaka wa : 2010-11


3. Edwin Van der Sar-Manchester United (Uholanzi)
Tuzo binafsi

Kipa bora wa mwaka Uholanzi: 1994, 1995, 1996, 1997
Mchezaji bora wa Ulaya : 1995, 2009
Timu ya mwaka ya ESM: 1995–96, 2008–09
Timu ya dunia ya All-Star: 1998 (Mchezaji wa Akiba)
Kiatu cha dhahabu nchini Uholanzi : 1998
Wawania kinyang'anyiro cha FIFA FIFPro World XI : 2006, 2007, 2008, 2009, 2010, 2011
Alikuwepo kwenye kikosi bora cha EPL mwaka : 2006–07, 2008–09, 2010–11
Mchezaji bora wa mechi michuano ya UEFA: Fainali 2007–08
Alikuwepo katika kikosi bora cha UEFA Euro 2008
Tuzo ya faida ya Barclays : 2008–09
Kipa bora wa EPL : 2008–09
UEFA Club Goalkeeper of the Year : 2009


2. Dino Zoff- Juventus (Italia)
Tuzo binafsi
Novemba 2003: Mchezaji bora wa Italy– Alikuwa ni mchezaji bora wa kizazi cha 50 iliyopita, ambapo alichaguliwa na Shirikisho la Soka Ulaya.
Mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or): 1973 (mshindi wa pili).
FIFA Order of Merit: 1984
UEFA European Championship Team of the Tournament: 1968, 1980
Timu ya wachezaji bora wa dunia wa UEFA: 1982
Kipa bora wa dunia wa FIFA: 1982
Tuzo ya mguu wa dhahabu 'Golden Foot'“Nguli wa soka”:2004
Mchezaji bora wa Italia "Hall of Fame': 2012


1. Manuel Neuer-Bayern Munich (Germany)
Tuzo binafsi 

Alipata tuzo ya medali ya fedha ya Fritz Walter kwa vijana chinya miaka 19 Silver 2005

tuzo ya Silbernes Lorbeerblatt: 2010

Mchezaji bora wa Ujerumani mwaka: 2011,2014

Alikuwepo timu ya mwaka ya ESM : 2011–12,2012–13

Alikuwepo timu ya UEFA Euro mwaka : 2012

Mchezaji bora wa fainali ya UEFA 2013 kwa upande wa mashabiki

Kipa bora wa dunia wa IFFHS: 2013, 2014

Kikosi bora cha FIFA/FIFPro : 2013,2014

Timu bora ya UEFA mwaka: 2013,2014

Kikosi cha timu bora ya UEFA cha msimu wa: 2013–14

Mchezaji bora wa pili wa UEFA: 2014

Kipa bora wa kombe la dunia mwaka: 2014

Alikuwepo kwenye kikosi bora cha 'FIFA World Cup All-Star' : 2014

WAKALI WENYE ,MAFANIKIO ZAIDI KATIKA KLABU MOJA LIGI KUU UINGEREZA HAWA HAPA

$
0
0
5. Jamie Carragher (Liverpool – michezo 737, magoli 5)
Beki huyo wa zamani England alicheza michezo 737 akiwa na Liverpool. Carragher (37) alishinda makombe mawili ya FA, kombe la vijana la FA, makombe mawili ya ligi na mawili ya ngao ya jamii. Pia alishinda kombe la ligi ya mabingwa Ulaya mara mbili, UEFA Cup na makombe mawili ya Super Cup.
Kwa ujumla alishinda makombe katika miaka yake 17 akiwa na Liverpool kuanzia mwaka 1996 mpaka 2013.


Gary Neville (Manchester United – Michezo 602, magoli 7)
Kocha huyo msaidizi wa timu ya taifa ya Uingereza kwa sasa, ni mwanachama wa United darasa la 92. Aliitumikia Man U kwa misimu 19 na kuchukua kila kombe ambalo mchezaji alihitaji kuwa nalo katika ngazi ya klabu. Beki huyo wa zamani ameshinda makombe 20, ikijumuisha makombe nane ya EPL, FA matatu, makombe mawili ya ligi, Matatu ya ngao ya jamii, moja la Intercontinental, kombe la dunia kwa vilabu na makombe mawili ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Alikipiga kwa Mashetani Wekundu kuanzia mwaka 1992-2011.


Tony Adams (Arsenal – Michezo 672, magoli 48)
Mchezaji huyo wa zamani wa Uingereza alitumia miaka yake yote ya soka kukipiga katika klabu ya Arsenal kama beki wa kati. Tangu mwaka 1983 mpaka 2002 akiwa na Arsenal, Adams alishinda makombe manne ya ligi kuu, makombe matatu ya FA, makombe mawili ya ligi, kombe la washindi la UEFA , na makombe matatu ya Ngao ya Jamii.
Katika maisha yake yote ya soka akiwa katika dimba la Highbury, Adams alikuwa nahodha wa Arsenal kwa takribani miaka 14.


Paul Scholes (Manchester United –  michezon 718, magoli 155 )
Akichukuliwa kama moja ya wachezaji wenye vipaji vikubwa sana kuwahi kutokea katika taifa la Uingereza. Katika misimu ishirini aliyochezea klabu ya Manchester United, Mpishi huyo wa mabao wa zamani wa England alichukua makombe yakiwemo makombe saba ya EPL, Matatu ya FA, mawili ya Ligi, matano ya ngao ya jamii, moja la Intercontinental Cup, moja la klabu bingwa ya dunia na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, pamoja na tuzo nyingine binafsi.


Ryan Giggs (Manchester United –michezo 963, magoli 168 )
Giggs ni mchezaji mwenye historia ya kipekee zaidi Uingereza baada ya kutumia miaka yake yote 24 ya soka kukipiga katika ligi kuu Uingereza kwenye klabu ya Man United.
Kiungo huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Wales ameshinda makombe 34 yakiwemo kumi na tatu ya Ligi Kuu Uingereza, manne ya FA, matatu ya Ligi, tisa ya Ngao ya Jamii, moja la UEFA Super Cup, moja la Intercontinental Cup, moja la Klabu Bingwa ya Dunia na mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Pia nashikilia rekodi ya klabu ya kuwa mchezaji aliyecheza michezo mingi zaidi na wa sita katika orodha ya wafungaji wa muda wote wa klabu.

ARGENTINA CHUPUCHUPU MBELE YA MEXICO, MESSI SHUJAA

$
0
0
Mexico walijikuta wakisalimu amri baada ya kushuhudia Argentina wakisawazisha magoli yote mawili  na kutoa sare ya magoli 2-2 katika mchezo wa kirafiki uliopigwa katika dimba la AT&T.
Sergio Aguero na Lionel Messi ndio walikuwa mshujaa kwa upande wa Argentina baada ya kufunga magoli hayo katika dakika za lala salama.
Arguero alifunga goli mnano dakika ya 85 na Messi alifunga katika dakika ya 89.
Mgoli a Mexico yalifungwa na Javier Hernandez (Chicharito) mnamo dakika ya 19 huku Hector Herrera akipachika bao la pili mnamo dakika ya 70.

WACHEZAJI WATANO WALIOPATA WAKATI MGUMU CHINI YA UTWALA WA MOURINHO

$
0
0
Jose Mourinho ni moja ya makocha wenye heshima kubwa sana katika ulimwengu wa soka, anajulikana kama "Special One" kama ambavyo mwenyewe pia hujiita.
Mourinho ametajwa kwenye orodha ya makocha watano walioshinda Kombe la UEFA akiwa na timu mbili tofauti, ambapo aliandika rekodi hiyo akiwa na Porto mnamo mwaka 2004 na Inter Milan mwaka 2010.

Lakini katika maisha yake ya ukocha akiwa klabu ya FC Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid, kuna baadhi ya wachezaji ambao waliteseka zaidi kutokana na uwepo wake.
Hapa kuna orodha ya wachezaji 5 ambao maisha yao ya soka yalikuwa machungu kutokana na Jose Mourinho:

Juan Cuadrado
Mkolombia huyu alikuwa mchezaji aliyecheza katika kiwango bora kwenye Kombe la Dunia mwaka jana nchini Brazili, ambapo alifunga bao moja na kutengeneza pasi 4 za magoli kwa timu yake ya taifa.
Cuadrado alijiunga na Chelsea akitokea klabu ya Fiorentina  ya Italia mwezi Februari mwaka huu na kusaini mkataba wa miaka minne na nusu kwa ada ya pauni milioni 23.3 huku Mohamed Salah akielekea huko huko kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.
Lakini alishindwa kuonesha makali yake katika dimba la Stamford Bridge chini ya kocha Jose Mourinho.

Juan Mata
Mata alijiunga na Chelsea akitokea kunako klabu ya Valencia mwaka 2011, alitoa mchango muhimu katika ushindi wa Chelsea wa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza pale alipotengeneza pasi kwa Didier Drogba katika fainali dhidi ya Bayern Munich na pia alishinda Ligi ya Europa na Kombe la FA akiwa na klabu hiyo.
Mnamo mwaka 2013, Mata, Oscar na Hazard waliunda safu ya ushambuliaji yenye nguvu katika Ligi Kuu ya Uingereza, na Mhispania akawa mchezaji bora wa Chelsea wa mwaka mara mbili mfululizo.
Tangu Jose Mourinho arudi Chelsea mwaka 2013, Mata aliishia kuwekwa bechi ilhali kocha akibaki kumtumia Oscar kama kiungo mshambuliaji wa kati na Andre Schurrle kama winga.
Baadaye mwezi Januari mwaka 2014, Mhispania huyo aliiondoka klabuni hapo na kujiunga na Manchester United.


Kaka
Baada ya kushinda tuzo mchezaji bora wa FIFA wa dunia mwaka vile vile kuchukua taji la Ligi ya Mabingwa akiwa na AC Milan, Kaka alijiunga Real Madrid kwa ada ya uhamisho Yuro 65,000,000 mwaka 2009, katika msimu wake wa kwanza akiwa Santiago Bernabeu, raia huyo wa Brazil alifanya vizuri.
Hivyo basi, wakati Jose Mourinho alipoteuliwa kuwa kocha mpya wa Madrid mwaka 2010, Kaka alianza taratibu kupoteza nafasi yake katika kikosi cha kwanza cha Madrid.


Mohamed Salah
Salah alikuwa akiangaliwa kwa jicho la karibu na vilabu kadhaa kutoka Ligi Kuu ya Uingereza baada ya ya kuwatungua Chelsea mabao mawili wakatia akiwa FC Basel katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, na ndipo Jose Mourinho alipomsajili raia huyo wa Misri kwa ada ya pauni milioni 11.
Tangu ajiunge na Chelsea mwezi Januari mwaka 2014, Salah aliishia kukaa benchi kabla ya kupelekwa kwa mkopo kunako klabu ya Fiorentina.


Iker Casillas
Casillas aliyeanza maisha yake ya soka katika timu vijana ya Real Madrid mwaka 1990 na kupanishwa kikosi cha kwanza mwaka 1999, tangu wakati huo, kipa huyo mzoefu aliisaidia Los Blancos kushinda mataji matano ya La Liga, mataji ​​mawili ya Copa Del Rey, mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa na vikombe vingi zaidi katika misimu kumi na sita.
Akiwa chini ya kocha Jose Mourinho, Casillas alianza kuwekwa benchi kwa kwa wababe hao wa Uhisapania katika mechi dhidi ya Malaga na kumtumia Antonio Adán kabla Mreno huyo kumsajili Diego Lopez kutoka Sevilla na kupata nafasi ya kudumu.
Hali hiyo ilileta huzuni kubwa nchini Hispania hasa kwa mashabiki wote wa Casillas baada ya kumwona kipa huyo maridadi akiishia kukaa benchi kwa muda mrefu.

KUELEKEA MSIMU MPYA WA LIGI, HII NDIO KAU;LI YA KOCHA MKUU WA AZAM

$
0
0
Azam FC inaendelea na mazoezi kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara ambapo kocha mkuu wa timu, Stewart Hall amepiga 'stop' kikosi chake kucheza mechi za kirafiki na sasa ni ufundi tu hadi msimu utakapoanza.
Stewart amesema, mechi 18 ambazo ni za kirafiki pamoja na za mashindano zimetosha kabisa kujua kipimo cha wachezaji wake.
"Kwa sasa ni ufundi tu, narekebisha mambo mengine madogo madogo,  hatutacheza tena mechi za kirafiki, nahitaji kuwa na kikosi changu kwanza kwa maandalizi zaidi,"Stewart aliiambia tvuti ya klabu ya Azam.
Katika mechi za kirafiki ambazo Azam FC wamecheza, wamepoteza mechi moja tu waliyofungwa na JKT Ruvu mabao 2-1 na nyingine walishinda pamoja na kutoa sare.
MECHI
Baadhi ya mechi walizocheza Azam waliifunga Friends Rangers  4-2, ilishinda mfululizo dhidi ya  JKT Ruvu 1-0 Chamazi, 1-0 African Sports Tanga, 1-0 na Coastal Union Tanga.
Katika mechi za Kombe la Kagame, Azam FC ilimaliza mechi zao zote bila kufungwa hadi ilipotangazwa bingwa. Iliwafunga KCCA 1-0, Malakia ya Sudan Kusini 2-0, 5-0 Adama City ya Ethiopia, Yanga SC penalti 5-3 baada ya kutoka suluhu tasa, KCCA 1-0 na mechi ya fainali dhidi ya Gor Mahia ya Kenya walishinda 2-0
Baada ya hapo ilijichimbia Zanzibar na kucheza mechi za kirafiki ikaifunga KMKM 1-0 , Mafunzo 3-0 na  JKU 2-0 kabla kupoteza kwa Yanga mchezo wao Ngao ya Hisani kwa penalti 8-7 baada ya suluhu.
Ilitoa sare ya 1-1 na Mwadui, na kufungwa na JKT Ruvu 2-1 .

ILIBAKI KIDOGO TU WENGER ATUE KWENYE KLABU HII, NA ANGEKUWA NA MAFANIKIO YA HATARI!!!

$
0
0
Alikuwa akiwindwa: Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon amefichua kuwa walitaka kumchukua Wenger miaka ya nyuma.
Arsene Wenger, ilibaki kidogo tu kutua Real Madrid - na hayo yangekuwa ni mafanikio yake makubwa sana katika kazi yake ya ukocha.
Rais wa zamani wa Real Madrid Ramon Calderon, amefichua kwamba walitaka kumchukua Wenger miaka ya nyuma lakini alikataa na kuamua kubaki Arsenal.
"Yeyote ambaye anafanya kazi katika sekta yoyote ile angependa kubadilisha mazingira. Nadhani ni wazo zuri kuwa na kocha ambaye ana mipango ya muda mrefu kwenye timu.
“Tulikuwa tukiongea kuhusu Real Madrid na, kwa wakati ule, alikuwa akivutiwa sana na klabu lakini nini kilitokea. Nakumbuka alisema: “Mnataka kwenda Hollywood tena, au kutengeneza timu ya soka?” Alimaanisha hivi mnataka kutengeneza filamu ya nyota wa Galacticos au kutengeza timu bora ya soka.
“Ni kitu kinachopatikana Uingereza ambacho ni kizuri sana kwa kweli. Kipo Arsenal, Manchester United pia, ambapo kocha anaweza kudumu klabuni kwa muda mrefu sana. Ni kitu kisichowezekana hapa.
“Nchini Uhispania, mashabiki na wafuasi wa Barcelona na Real Madrid, wanachohitaji wao ni ubingwa na makombe tu. Lakini nchini Uingereza, ni kitu ambacho wanafanya vizuri sana –kumpa kocha sapoti na kumfanya najiamini. Kuweka uhusiano mzuri kati ya kocha na klabu. Wenger ni uthibitisho wa hilo.
“Kwa hiyo hatukuweza kufanikiwa kumleta na amependa sana maisha ya pale Arsenal… Wenger ... ni mtu mwenye heshima kubwa sana. huwezi kumkuta akibisha hovyo. Kuna baadhi ya nyakati ndio husikia akilaumu waamuzi lakini sio kama ambavyo Mourinho hufanya.
“Wenger ni mtu mwema sana. Ni kocha mwenye muonekano wa kipekee, mtu mzuri na ninafurahi sana kumuona akiwa amefanikiwa, lakini pia nadhani angekuwa mtu bora sana kwa klabu ya Madrid. Japokuwa Madrid ni klabu yenye ugumu wa aina yake wakati mwingine.
“Hebu ona yaliyomtokea Mourinho. alishinda kila kitu pale lakini. Pia kwa Capello… alipata mafanikio makubwa, lakini mashabiki hawakuwa na furaha na jini timu yao ilivyokuwa ikicheza na ndipo tulipolazimika kumtimua… Pia tatizo kama hilo lilikuwa kwa Mourinho.
“Arsene Wenger si aina ya makocha hao. Timu yake hupenda kucheza soka la kuvutia kwa mashabiki lakini pia kwa wadau wengine.
“Lakini hata hivyo tatizo bado ni hilo hilo tu. Ni vigumu sana kudumu na kocha kwa miaka hata mitatu tu. Presha huwa iko juu sana kutoka kwa mashabiki. Pia ni vigumu sana kuendana na presha ya vyombo vya habari.
“Ni hatari sana kama kocha haleti matokeo na hata kama akishinda basi hachezi mtindo ambao mashabiki hupendelea, hiyo inakuwa bado changamoto kubwa sana. Pengine angeweza kupata mafanikio, lakini kama unakuja hapa kuna mengi sana ya kuyatatua”.

YANGA YAJA KIVINGINE

$
0
0
KLABU ya Yanga imeamua kuja kivingine msimu huu ikitaka kuzichanganya timu watakazokutana nazo kwa ‘style’ mbalimbali za uchezaji lakini zaidi ikiwa ni ufungaji mabao.
Kocha Mkuu wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm, amekuwa akisifika kwa mtindo wake wa soka la kushambulia kuanzia dakika ya kwanza hadi ya mwisho.
Mfumo huo ndio hasa unaomwezesha Pluijm kupata ushindi mnono kama ilivyokuwa msimu uliopita ambapo alikuwa akishinda hadi mabao 8-0 kama alivyoifanya Coastal Union katika mchezo wa marudiano kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa timu hiyo raia wa Zimbawe, Donald Ngoma, ndiye aliyevujisha mkakati wao huo akisema katika kuusapoti kwa vitendo, wataanza na mtindo wa kufunga mabao ya mapema zaidi kabla timu pinzani hazijajipanga vizuri ili kuzichanganya.
Akizungumza na BINGWA, Ngoma alisema kuelekea mchezo wao wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara Jumapili dhidi ya Coastal Union kwenye Uwanja wa Taifa, Ngoma aliyetua Yanga msimu huu akitokea FC Platinum ya Zimbabwe, alisema moja ya mikakati yake ni kuweka rekodi kuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kufunga bao la mapema zaidi.

LISTI WA WACHEZAJI WENYE SPIDI ZAIDI DUNIANI IPO HAPA

$
0
0
Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcott, ndio mchezaji anayeongoza kwa kasi awapo uwanjani akiwa na spindi ya 96. Kiungo wa klabu ya Fortuna Dusseldorf mwenye umri wa miaka 24 Mathis Bolly pia ana kasi ya 96, huku winga wa BorussiaDortmund Emerick Aubameyang akipata 95. 

Hii ndio ishirini bora ya wanaoongoza kwa spidi kwa mujibu wa Metro.
1. Theo Walcott (Arsenal) – 96
2. Mattis Bolly (Fortuna Dusseldorf) – 96
3. Pierre-Emerick Aubameyang (Borussia Dortmund) – 95
4. Ernest Asante (Stabaek Fotball) – 95
5. Jurgen Damm (Tigres Uanl) – 95
6. Gareth Bale (Real Madrid) – 94
7. Jonathan Biabiany (Inter Milan) – 94
8. Dominic Oduro (Impact De Montreal) – 94
9. Kekuta Manneh (Vancouver) – 94
10. Marco Sau (Cagliari) – 94
11. Innocent Emeghara (San Jose) – 94
12. Fahad Al-Muwallad (Al-Ittihad) – 94
13. Ryo Miyaichi (St. Pauli) – 94
14. Lucas (Paris Saint-Germain) – 93
15. Juan Cuadrado (Juventus) – 93
16. Raheem Sterling (Manchester City) – 93
17. Luciano Narsingh (PSV) – 93
18. Maicon (Lokomotiv Moscow) – 93
19. Ahmed Musa (CSKA Moscow) – 93
20. Bruma (Real Sociedad) – 93

Hata hivyo, hakuna nafasi kwa mchezaji mwenza wa Walcott Hector Bellerin, ambaye ndio anasemekana kuongoza kwa spidi katika klabu ya Arsenal kwa mujibu wa takwimu zilizochukuliwa klabuni hapo mwezi Februari. 

Orodha ya wachezaji 16 bora ya FIFA inatarajiwa kutoka tarehe 22 September.

SABABU GANI ZILIZOMFANYA WENGER ASISAJILI?ZIPO HAPA KAZITOA MWENYEWE

$
0
0
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger, ametoa utetezi wake juu ya kushindwa kununua mchezaji wa ndani katika dirisha la usajili lililofungwa hivi karibuni, akisema kuwa hakukuwa na mchezaji ambaye klabu ilikuwa na uhitaji naye.
Vijana hao wenye maskani yao kwenye jiji la London, walimsajili kipa Petr Cech tu kutoka Chelsea mapema kabisa wakati dirisha la usajili limefunguliwa, hali iliyojenga imani kubwa kwa mashabiki juu ya ubingwa wa EPL msimu huu, lakini hata hivyo hakuna usajili mwingine uliofanyika.
Wenger alihusishwa na tetesi za kumsajili mshambulaiji wa Real Madrid Karim Benzema lakini hata hivyo mpaka dirisha linafungwa hakuna kilichotokea.
Wenger aliwaambia waandishi: "Mwishoni, suluhisho lilikuwa si kama tulivyaka. Tuliangalia kwa makini lakini hakukuwa na suluhisho sahihi.
"Hebu angalia katika soko la wachezaji kwa sasa, utaona kwamba kuna upungufu mkubwa sana wa wachezaji. Suluhisho tulilokuwa nalo halikuwa na ushawishi kabisa.
"Habari njema kuhusu dirisha ka usajili, sasa limefungwa rasmi na tunachokiangalia kwa sasa ni kucheza mpira tu".

PIGO KUBWA KWA CHELSEA KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA EVERTON

$
0
0
Wasiwasi kwa Thibaut Courtois kuivaa Everton wikiendi hii.
Thibaut Courtois yuko hatarini kuukosa mchezo wa ligi mwishoni mwaka wiki hii pale timu yake ya Chelsea itakapokuwa ugenini kucheza na Everton baada ya kupata jeraha la goti wakati akiwa mazoezi.
Mlinda mlango huyo namba moja wa Ubelgiji arudi mzima baada ya kutoka kuitumikia timu yake ya taifa lakini alijiumiza mwenyewe wakati wa mazoezi katika dimba la Cobham jana.
Courtois alipata jerahala goti wakati wa maandalizi ya mchezo dhidi ya Swansea lakini alirejea uwanjani kabla ya baadaye kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Kutokana na hali hiyo, kipa namba mbili wa klabu hiyo 
Asmir Begovic anatarajiwa kukaa langoni mwa Chelsea katika mchezo huo mgumu ambao Chelsea wanasaka pointi tatu kwa udi na uvumba ili kurejea katika nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi.

MICHUANO YA FA YAREJEA NCHINI, SHUGHULI YAWEZESHA NA AZAM MEDIA, ZIJUE TIMU ZITAKAZOSHIRIKI

$
0
0
Rias wa TFF Jamal Malinzi (kulia) akiwa na 
Afisa Mtendaji Mkuuwa Azam Media, Rhys Torrington wakati wa makabidhiano ya mkataba wa kuanza michuano ya Ligi
Ya FA

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kwa kushirikiana na Azam Media, wameanzanisha michuano ya Mpira miguuu itakayojulikana kwa “Azam Sports Federation Cup” 
Shindano la hilo litatumia mfumo maarufu ambao unatumiwa nchini Uingereza katika michuano ya FA na vilevile nchini Uhispania katika michuano ya Copa del Rey nchini Hispania.
Akizindua Shindano hilo jpya kabisa wakati wa hafla fupi iliyofanyika jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na viongozi mbali mbali wa Kampuni ya Azam Media na wamiliki wa timu za mpira nchini kutoka madaraja yote, Malinzi amesema michuano hiyo itazishirikisha timu mbalimbali ikiwemo za Ligi Kuu ya Vodacom na timu za madaraja mengine mawili ya chini na kufanya idadi ya timu kufikia 54.
Malinzi amesema michuano hiyo itakuwa na msisimko mkubwa nchini na itakuwa huku lengo lake kubwa likiwa ni kuinua soka ambalo kimsingi limeshuka kutokana na ligi kuu kukosa timu nyingi.
Michuano hii itakuwa chachu katika kuleta msisimko wa Watanzania, hasa ukizingatia kwamba kwa kipindi kirefu wamekuwa wakitaka michuano kama hii ambayo inashirikisha timu za Ligi kuu pamoja na ligi daraja la kwanza na la pili ili kuleta hamasa katika mikoa ambayo haina timu inayoshiriki ligi kuu", alisema.
Malinzi ameongeza kuwa timu itakayochukua kombe hilo itajinyakulia kitita cha shilingi za Kitanzania milioni 50 pamoja na kupata nafasi ya kushiriki moja kwa moja kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Amesema endapo timu ambayo ipo ligi kuu itashika nafasi ya 1 kwenye msimamo wa Ligi, na pia ikafanikiwa kuchukua kombe la FA basi nafasi hiyo itapewa na Timu ambayo itaingia fainali kwenye michuano ya FA.
Kwa Upande wake Afisa Mtendaji Mkuuwa Azam Media Rhys Torrington,  amesema nia ya Kampuni yake kudhamini michuano hiyo ni kutaka kukuza mpira nchini kwa kutaka kufikia malengo.
Amesema licha ya kudhamini michuanao hiyo kwa kipindi cha Miaka 4, pia michuano hiyo itarushwa moja kwa moja kupitia Vituo vya TV vya Azam Media.
Udhamini utagharimu kiasi cha bilioni 3.3 kwa kila mwaka.
TIMU ZITAKAZOSHIRIKI HIZI HAPA
17-24 RED TEAMS
1. PANONE FC – KILIMANJARO
2. POLISI DAR-ES-SALAAM –DAR-ES-SALAAM
3. POLISI – DODOMA
4. POLISI MARA –MARA
5. POLISI MOROGORO –MOROGORO
6. POLISI TABORA –TABORA
7. RHINO RANGERS – TABORA
8. RUVU SHOOTING – PWANI
9. MVUVUMA FC – KIGOMA
10. PAMBASC – MWANZA
11. SABASABS UNITED FC – MOROGORO
12. SINGIDA UNITED – SINGIDA
13. TRANSIT CAMP – DAR-ES-SALAAM
14. TOWN SMALL BOYS – RUVUMA
15. VILLA SQUAD – DAR-ES-SALAAM
16. WENDA SC – MBEYA


1-16 BLUE TEAMS
1. ABAJALO FC – DAR-ES-SALAAM
2. ABAJALO FC – TABORA
3. AFC – ARUSHA
4. ALLIANCE SCHOOLS FC – MWANZA
5. CHANGANYIKENI – DAR-ES-SALAAM
6. COCACOLA KWANZA FC –MBEYA
7. COSMOPOLITNI FC – DAR-ES-SALAAM
8. GREEN WORRIORS FC –DAR-ES-SLAAM
9. JKT RWAMKOMA FC
10. KARIAKOO SC – LINDI
11. MADINIS SC –ARUSHA
12. MAGEREZA –IRINGA
13. MKAMBA RANGERS FC – MOROGORO
14. MILAMBO SC – TABORA
15. MSHIKAMANO SC – DAR-ES-SALAAM
16. BULYANHULU FC – SHINYANGA
CREDIT:fullhabari

MESSI NA RONALDO SI WATU WAZURI HATA KIDOGO, ANGALIA TAKWMU ZAO ZA MICHUANO YA ULAYA HAPA

$
0
0
Lionel Messi na Cristiano Ronaldo wote kwa pamoja wana magoli 80 katika michuano ya Ulaya – lakini je, kila mmoja amefunga kuoka eneo gani? je, kutoka upande gani (kushoto ama kulia)? ndani ya boksi au nje ya boksi? dhidi ya nani (timu gani)? Takwimu zote zipo hapa

HAWA NDIO WACHEZAJI WATANO BORA AMBAO VAN GAAL AMEWAHI KUWAFUNDISHA

$
0
0
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal amemtaja Wayne Rooney katika orodha ya wachezaji matano bora ambao amewahi kuwafundisha katika maisha yake ya soka.
Akizungumza katika hafla moja uliyoandaliwa na mashabiki wa timu hiyo juzi usiku, Van Gaal, ambaye amewahi pia kuzifundisha timu za AZ, Ajax, Barcelona, Uholanzi na Bayern Munich, amemsifu Rooney kuwa ndiye nahodha bora kati ya manahodha wote aliwahi kuwa nao na kutoa orodha hiyo ya wachezaji watano bora ambao amewahi kufanya nao kazi...

WAYNE ROONEY


LUIS FIGO


RONALD DE BOER


PHILIPP LAHM


BASTIAN SCHWEINSTEIGER

KOCHA BORA,MCHEZAJI BORA WA MWEZI EPL WATANGAZWA

$
0
0
Kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini, ametajwa kuwa kocha bora wa mwezi Agosti wa Ligi Kuu nchini Uingereza.
City ndio timu pekee ambayo mpaka sasa imeshinda michezo yake yote huku ikiwa haijaruhusu hata bao moja kutikisa nyavu zake.
Katika kinyang'anyiro hicho, Pellegrini amewashinda makocha wenzake Alan Pardew (Crystal Palace), Garry Monk (Swansea) na Claudio Ranieri.
Wakati huo huo, kiungo mshambuliaji wa Swansea Mghana Andre Ayew ameshinda tuzo ya mchezaji bora, baada ya kufunga magoli matatu katika michezo yake minne, huku ukiwa ndio msimu wake wa kwanza kabisa EP akitokea Ufaransa kunako klabu ya Marseille.

MLINZI HUYU WA MAN U ANAMUOGOPA VAN GAAL BALAA!!!

$
0
0
Beki wa Manchester United Muargentina Marcos Rojo, amekiri kutishwa na uso wa kocha wa klabu hiyo Luis Van Gaal, akiufananisha na 'uso wa mbwa mkali'
Mapema kabisa wiki hii kulikuwa na taarifa kuwa wachezaji waandamizi wa klabu hiyo kuhusu mbinu zake ngumu za ufundishaji ambazo zinawapa wakati mgumu wachezaji hao.
Rojo, ambaye mpaka sasa hajacheza hata mchezo mmoja tangu ufunguzi wa ligi, hakujumuika na timu yake wakati wa maandalizi ya msimu mpya (pre-season) kutokana na tatizo la pasi yake ya kusafiria (passport).
"Ana muonekano unaotisha kwa kweli, lakini bado ni mtu mzuri tu. Ana uso wa mbwa, lakini ni mtu safi sana, mwanzo ukimuona unaweza kumkimbia, lakini kadri unavyomzoea unaona utofauti, lakini hiyo, ni endapo utamsikiliza anachokwambia," alisema Rojo.
Mshambulizi wa zamani wa United Diego Forlan amedai kuwa Van Gaal "kamwe hajawahi kuwa na mapenzi na wachezaji wenye asili ya Amerika ya Kusini" lakini Rojo amesisitiza kuwa hajawahi kufanyiwa baya lolote na Mdachi huyo.
"Labda hali hiyo inatokana na mahusiano yake mabaya na Roman [Riquelme] au Angel di Maria ambaye ameondoka, watu wengine wana mtazamo tofauti kabisa, lakini ninachoona mimi hapa ni kwamba wote anatupa usawa".

POZI LA FABREGAS ENZI HIZO AKIWA NA VAN GAAL LA MASIA

$
0
0
Kiungo wa Chelsea Cesc Fabregas ameposti picha yake ya utotoni kwenye Instagram, wakati akiwa katika akademi ya Barcelona maarufu kwa jina la La Masia.
Picha hiyo vile vile inamuonesha kocha wa sasa wa Manchester United Louis van Gaal, ambaye amewahi kuwa kocha wa Barcelona miaka ya nyuma, pamoja na beki wa Barcelona Gerard Pique.
Fabregas alikuwa mwanafunzi katika akademi hiyo wakati akiwa na miaka 10 kabla ya kwenda Arsenal hapo baadaye mwaka 2003.

PIGO KUBWA KWA CHELSEA KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA EVERTON KESHO

$
0
0
Chelsea wamepata pigo kubwa baada ya kipa wao Thibaut Courtois kupata jeraha la goti litakalomuweka nje kwa takribani miezi miwili.
Thibaut Courtois anatarajiwa kuwa nje kwa takribani miezi miwili kutokana na jeraha la goti.
Hilo ni pengo kubwa kwa kocha wa klabu hiyo Mourinho, hasa kutokana na kuwa na mwanzo mbaya kwa timu yake kwenye ligi, baada ya kufungwa michezo miwili, kutoka sare mmoja na kushinda mmoja.

ROONEY HUMPA WAKATI MGUMU VAN GAAL KWA HILI HAPA!!

$
0
0
Kocha wa Manchester United Louis van Gaal, amekiri kwamba humuwia vigumu sana kuelewa pindi anapozungumza na nahodha wake Wayne Rooney .
Van Gaal amemsifu Rooney na kusema kuwa ni moja ya wachezaji watano bora ambao amewahi kuwafundisha katika maisha yake ya soka.
Alipoulizwa kuhusu kuelewana vyema na Rooney, Van Gaal alijibu, lafudhi ya Rooney humpa wakati mgumu sana pindi wanapowasiliana.
"Wakati nikiongea, huwa natamka maneno vizuri tu”, Van Gaal aliiambia RTL4’s 'Linda's Zomerweek’.
“Kama ukimuweka Wayne Rooney katika siti hii, na ukaanza kuzungumza naye, unadhani kuwa watu watamuelewa Wayne Rooney? huwezi kumuelewa kamwe anachokizungumza".

HII NDIO SALARY MPYA YA DAVID DE GEA BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MIAKA 4

$
0
0
Baada ya David De Gea kuonekana na wakala wake maeneo ya viwanja vya Manchester united hatimaye kazi iliyowapekela imekamilika baada ya De Gea kusaini mkataba miaka 4 na huu ndio mshahara wake.
Mchezaji huyu mwenye miaka 24 atakua analipwa £200,000 kila wiki na kwa kiasi kikubwa anategemewa kuanza kwenye mechi ya kesho dhidi ya Liverpool. David De Gea ilibidi ajiunge na Real Madrid kwa gharama ya pound million 29 lakini dili hilo lilishindikana kwenye dakika za mwisho.

KAULI YA WENGER BAADA YA KUAMUA KUTOSAJILI MSHAMBULIAJI MSIMU HUU

$
0
0
Arsenal hawana tatizo la katika safu yake ya ushambuliaji, hayo ni maneno ya Arsene Wenger ambaye pia anasema uwepo wa Alexis Sanchez, Olivier Giroud na Theo Walcott, unaweza kumpa magoli zaidi ya 20 kwa msimu. 
Arsenal walihusishwa na usajili wa Karim Benzema na Edinson Cavani, lakini hata hivyo mambo yalikwenda ndivyo sivyo na badala yake kuamua kutonunua mshambuliaji yeyote.
“Nadhani Giroud, Walcott na Sanchez wanaweza kuleta magoli zaidi ya 20 bila tatizo lolote lile", aliwaambia waandishi. 
"Wakati mwingine lazima uwaamini wachezaji wako na kuwapa nafasi. Halafu baada ya muda watafanya vyema tu. Mara nyingi watu hutaka mafanikio ya haraka, lakini hatuendi hivyo.
“Nina Aaron Ramsey ambaye anaweza kufunga magoli 15, Mesut Ozil 15, Santi Cazorla 10. Vinginevyo, kama una mchezaji mmoja ambaye ndiye unategemea kwa ufungaji, siku akipata majeraha je?, nani atafunga sasa”.
Wenger amekosolewa kwa kutosajili mshambuliaji mpya katika dirsha la usajili lililofungwa mapema mwezi huu, lakini alilisisitiza kuwa kwa sasa washambuliaji hawapatikani tena katika bara la Ulaya.
"Washambuliaji wengi wanapatika nara la Amerika ya Kusini kwa sasa. Bara la Ulaya hawazalishi washambuliaji siku kabisa.
"Angalia nchi kama Ujerumani, ambayo ilicheza dhidi ya Scotland au dhidi ya Poland huku Mario Gotze ndio akiwa mshambuliaji wa mwisho – huyu ni kiungo. Si kana kwamba hawataki kumchezesha mshambuliaji halisi pale mbele lakini hayupo mshambuliaji ambaye ana vigezo vya kusimama pale mbele.
"Nani ambaye unamuona hapa Ulaya?"
"Kitu ninachoweza kusema ni kwamba, katika hizi akademi za soka zinatakiwa kuwatenegeneza washambuliaji tangu wakiwa katika umri mdogo. Kuna umri kati ya miaka mitano mpaka 12 ambapo ndipo unaweza kutengeneza kipaji cha maana. Umri katika ya miaka 12-14 unaanza kumtengeza katika kasi yake na nguvu katika mwili.
Viewing all 1447 articles
Browse latest View live