Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all 1447 articles
Browse latest View live

WENGER AENDELEZA FALSAFA ZAKE ZA VIJANA, HUYU HAPA KAMPA NAFASI KATIKA KIKOSI CHA UCL ARSENAL

$
0
0
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger amemjumuisha mchezaji Jeff Reine-Adelaide katika kikosi chake kitakacho shiriki michuano ya Champions League.
Mfaransa huyo mwenye miaka 19, aliyesajiliwa akitokea Lens ya Ufaransa, alicheza vizuri katika maandalizi msimu huu hasa katika Emirates Cup mwezi July.
Pia Arsenal imechagua vijana saba kutoka kikosi B kwa ajili ya mashindano.
Arsenal imepangwa kundi F pamoja na timu za Bayern Munich, Olympiacos na Dinamo Zagreb katika michuano ya Champions League. 

SAMATA, NGASA, ULIMWENGU KAMILI GADO KUWANYOSHA NIGERIA....

$
0
0
Wachezaji watatu wa kimataifa wa Tanzania wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi, Mrisho Ngasa (Free State – Afrika Kusini) , Thomas Ulimwengu na Mbwana Samatta (TP Mazembe – Congo DRC) wamejiunga na kambi ya Taifa Stars iliyopo katika hoteli ya Urban Rose – Kisutu jana jijini Dar es salaam.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars Charels Mkwasa amewapokea wachezaji hao na kufanya mazoezi ya pamoja na wachezaji waliokuwa kambini nchini Uturuki saa 10 jioni katika uwanja Taifa jijini Dar salaam.
Kwa mujibu wa ratiba ya kocha Mkwasa Stars leo alhamis ataendelea na mazoezi jioni saa 10 katika uwanja wa Taifa kabla ya kufanya mazoezi mepesi ya mwisho kesho Ijumaa asubuhi.
Wachezaji waliopo kambini ni magolikipa Ally Mustafa, Said Mohamed, walinzi Juma Abdul, Shomari Kapombe, Haji Mwinyi, Mohamed Hussein, Kelvin Yondani, Hassan Isihaka na nahodha Nadri Haroub “Cannavaro”.
Viungo ni Himid Mao, Frank Domayo, Mudathir Yahya, Said Ndemla, Salum Telela, Deus Kaseke, Saimon Msuva na Farid Musa, huku safu ya ushambuliaji ikiwa na John Bocco, Rashid Mandawa, Ibrahim Ajib, Thomas Ulimwengu, Mrisho Ngasa na Mbwana Samatta.

KWA MKWANJA HUU UTAZIONA STARS, SUPER EAGLES JUMAMOSI

$
0
0

Baraka Kizuguto, Afisa habari wa TFF

Maandalizi ya mchezo kati ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya Nigeria (Super Eagles) yamekamilika, ambapo leo Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo huo wa Jumamosi ambapo kiingilio cha chini ni shilingi elfu saba tu.
Viingilio vya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON Qaulifier 2017) kundi G viitakuwa ni VIP A Tsh 40,000, VIP B Tsh 30,000, VIP C Tsh15,000, Rangi ya Machungwa (Orange) Tsh 10,000, na viti vya rangi ya Bluu na Kijani Tsh 7,000.
Tiketi za mchezo huo zinatarajiwa kuanza kuuzwa kesho Ijumaa saa 4 kamili asubuhi katika vituo kumi vifuatavyo:
(i) Ofisi za TFF - Karume
(ii) Buguruni – Oilcom
(iii) Mbagala – Dar live
(iv) Ubungo – Oilcom
(v) Makumbusho – Stendi
(vi) Uwanja wa Taifa
(vii) Mwenge – Stendi
(viii) Kivukoni-  Feri
(ix) Posta – Luther House
(x) Big Bon – Msimbazi Kariakooo
TFF inawaomba watanzania, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu kununua tiketi za mchezo huo katika magari yaliyopo kwenye vituo vilivyotajwa ili kuondokana na tatizo la kuuziwa tiketi zisizokuwa halali.
Jeshi la Polisi nchini kwa kushirikiana na idara nyingine za kiusalama wameandaa usalama wa kutosha kuelekea  mchezo huo.
Mchezo huo utaanza saa 10:30 jioni kwa saa za Afrika Mashariki ikichezeshwa na waamuzi kutoka nchini Rwanda ambao wanatarajiwa kuwasili leo jioni pamoja na kamisaa wa mchezo huo.
Waamuzi wa mchezo huo ni Louis Hakizimana (mwamuzi wa kati) Honore Simba (mwamuzi msaidizi), Jean Bosco Niyitegeka (mwamuzi msaidizi), Abdoul Karim Twagiramukiza (mwamuzi wa akiba) wote kutoka Rwanda na kamisaaa ni Charles Kasembe kutoka nchini Uganda.

JOHN BOCCO: “TUTAPIGANA KUISHINDA NIGERIA JUMAMOSI”

$
0
0
John Bocco ‘Adebayor’ mshambuliaji wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na Azam FC
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam 
Mshambulizi wa Taifa Stars, John Bocco amesema wachezaji wote wapo tayari kwa gemu ya Jumamosi hii dhidi ya Nigeria katika kuwania tiketi ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika 2017. Stars itaikaribisha ‘Super Eagles’ katika uwanja wa Taifa.
“Kwa upande wetu sisi kama wachezaji tuko tayari kwa mechi. Tumefanya maandalizi mazuri, mwalimu amekuwa akitupatia mbinu tofauti za kuweza kuwakabili Nigeria. Wachezaji tumekuwa tukimsikiliza na kuyafanyia kazi maelekezo yake. Kwanza nitangulize shukrani zetu kama wachezaji kwa mashabiki wetu”, amesema Bocco.
“Kabla ya kucheza na Uganda (kufuzu CHAN) tulikuwa tukipigwa na mawe, tunazomewa kila tunapopita. Watanzania walikata kabisa tamaa na timu yao ya Taifa lakini sasa tunaona wamerudisha moyo wao na tunachoweza kuwaambia wasivunjike moyo, watuamini kama wanavyotuamini kwa sasa, tutapigana Jumamosi ili kushinda gemu yetu”.

HIVI NDIVYO MBWANA SAMATTA ALIVYO SILAHA MUHIMU STARS

$
0
0

Mwana Samatta, mshambuliaji wa kimataifa wa timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na timu ya TP Mazembe ya Congo DRC
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam 
Alifunga magoli 16 katika ligi daraja la kwanza Tanzania Bara mwaka 2008 wakati akiwa na miaka 16 tu. Mwaka mmoja baadae akafunga magoli sita wakati alipocheza ligi kuu Bara kwa mara ya kwanza msimu wa 2008/09 akiwa na timu ya African Lyon.
Mbwana Samatta alipanda chati ghafla mara baada ya kuanza kuichezea Simba SC katika michezo ya mzunguko wa pili katika ligi kuu bara msimu wa 2010/11. Alifunga magoli nane katika gemu 12 za ligi na magoli mengine matatu katika gemu nne za klabu bingwa Afrika.
Samatta ni mshambulizi hatari, ana uwezo wa dribbling kwa kasi, kupiga chenga, mashuti na uwezo wa kutengeneza nafasi za magoli. Alisajiliwa na TP Mazembe Mei, 2011 na akawa maarufu zaidi jijini Lubumbashi wakati alipofunga magoli sita katika michuano yake ya kwanza ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka 2012 wakati TP ilipofika hatua ya nusu fainali.
Samatta aliondoka Tanzania akiwa na miaka 18 na hadi sasa amecheza zaidi ya mechi 103 na kufunga mara 60 katika timu hiyo bingwa mara nne wa kihistoria barani Afrika. Huyu ni mchezaji wa kiwango cha dunia tena bahati anatoka nyumbani Tanzania.
Amekuwa sehemu ya wachezaji wa timu ya Taifa Stars tangu mwaka 2011 wakati alipoitwa na kufunga katika mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, AFCON 2012. Alifunga magoli mawili katika harakati hizo za Stars ambazo zilishindwa kufanikiwa. Akiwa tayari ameichezea Stars mara 27, rekodi ya Samatta katika ufungaji si nzuri akiwa na Stars. Ameifungia Stars mara tisa tu.
Kila inapofika mechi ya Stars wapenzi wa mpira nchini wamekuwa na matarajio ya kumuona mfungaji wao wa mipira ya kichwa na mashuti akifunga lakini mambo yamekuwa tofauti. Atakuwa anafuatiliwa kila kitu na benchi la ufundi la Nigeria na watamuandalia mikakati mikubwa kuhakikisha wana mzima.
Dhidi ya Nigeria itakuwa mechi ya kipekee kwake kwani anacheza na timu ambayo Ahmed Musa yupo. Samatta, 23, alishakwenda CSKA Moscow ya Urusi kwa ajili ya kufanya majaribio wakati Musa ndiye staa wa sasa wa ufungaji katika klabu hiyo ya Urusi.

NDEMLA, AJIB KUWALAZIMISHA MASHABIKI WA YANGA KUWASHANGILIA

$
0
0
SAID Ndemla na Ibrahim Ajib ni miongoni mwa wachezaji wa Simba waliopo katika kikosi cha Taifa Stars ambao kesho watabadili msimamo wa mashabiki wa Yanga kwa kuwashangilia watakapoivaa Nigeria kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Simba na Yanga zenye upinzani wa jadi zimekuwa na uhasama wa muda mrefu ambapo zimekuwa hazitakiani heri mojawapo inapocheza na timu nyingine.
Uhasama baina ya timu hizo umekuwa ukiendelea hata kwa wachezaji mmoja moja hata pale anapokuwa katika majukumu ya timu ya Taifa.
Mathalani, mchezaji wa Yanga aliyepo Taifa Stars anapoboronga au kutolewa wakati timu hiyo inapocheza na timu yoyote, huzomewa mno na mashabiki wa Simba.
Hali huwa hivyo pia kwa mchezaji wa Simba anapofanya vibaya akiwa Stars kwa kujikuta katika wakati mgumu mbele ya mashabiki wa Yanga.
Lakini katika kile kinachoonekana mashabiki wa soka Tanzania kufahamu maana na neno ‘kuweka silaha chini’, wale wa Yanga wametangaza rasmi kuweka kando uhasama wao wa jadi na Simba kwa kuwashangilia wachezaji wa Wekundu wa Msimbazi hao waliopo Stars katika mchezo wa kesho.
Wakizungumza na BINGWA Dar es Salaam jana, mashabiki hao walisema wana kila sababu ya kwenda kwa wingi Uwanja wa Taifa kuishangilia Stars, wakisisitiza kuonyesha uzalendo wa hali ya juu kuishangilia Stars inayonolewa na mzalendo, Charles Boniface Mkwasa.

HUU NDIO USAJILI MBOVU KABISA KATIKA DIRISHA LA USAJILI MWAKA 2015 (TOP 5 WORST SIGNING SUMMER-2015)

$
0
0
5. Radamel Falcao. Kutoka AS Monaco kwenda Chelsea.
Alikuwa na msimu mbovu alipokuwa Manchester United msimu uliopita licha ya kupewa nafasi kubwa ya kucheza. Aliishia kufunga mabao manne tu. Lakini Mourinho ameamua kumleta vivyo hivyo akiamini ataisaidia timu yake.

4. Papy Djilobodji. Pauni milioni 2.2
Kutoka Nantes kwenda Chelsea.
Ripoti mbalimbali kutoka nchini Ufaransa zinaeleza kuwa hakuna chochote ambacho beki huyo anaweza kuwapa Chelsea. Iliripotiwa kuwa alitaka kupelekwa katika vilabu mbalimbali vya Uingereza lakini alikataliwa licha ya bei yake kuwa ndogo. Kwa uwezo uwanjani wataalamu wanasema hana kiwango cha kuwashinda Zouma,Cahill au mlinzi mwingine yeyote wa Chelsea.


3. Fabian Delph. Kutoka Aston Villa kwenda Manchester City.
Mwanandinga huyu hana uwezo wa kuwashinda Yaya Toure, Silva,Fernadihno, Navas,Fernando, Sterling,Debruyne na hata Nasri, ndio maana mpaka sasa tunaweza kusema kuwa hana nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza kwa City.


2. Younes Kaboul. Kutoka Tottenham Hotspur kwenda Sunderland.
Sunderland walikuwa na tatizo kubwa katika safu ya ulinzi msimu uliopita. Waliruhusu magoli mengi sana ambayo yangeweza kuwasababisha kushuka daraja. John Oshea na Wes Brown kwa sasa wakati umeshaanza kuwatupa mkono, Sasa usajili wa Kaboul mwenye miaka 29, ambaye pia ni ni mwepesi wa kuapata majeraha ya mara kwa mara ni tatizo jingine.

1. Bastian Schweinsteiger - Yuro milioni 14. Kutoka Bayern Munich kwenda Manchester United
Bastian Schweinsteiger anaweza kuwa moja ya wachezaji wenye uzoefu mkubwa katika klabu ya Manchester United kwa msimu huu, lakini sio wa kucheza katika kikosi cha kwnza kwa dakika zote . Kwa sasa Bastian ana umri wa miaka 30. Mechi dhidi ya Swansea na Newcastle zilithibitisha hilo. Badala yake Bayern Munich waliamua kumsajili Arturo Vidal kuziba pengo lake, Vidal ni mchezaji ambaye United walikuwa wakihusishwa naye wakatika wa dirisha la usajili la mwezi January.

WACHEZAJI 10 BORA WANAOONGOZA KUWA NA MASHABIKI WENGI TWITTER NA KUJIKUSANYIA PESA NYINGI

$
0
0
Ndio maana sio suala la kushangaa ama kuuliza kwa nini Cristiano Ronaldo aliamua kutumia akaunti yake ya Twitter kuitangaza kampuni moja ya ushonaji ya nchini Ureno, vile vile kwa nini Wayne Rooney aliamua kuposti picha ya Nike katika viatu vya kuchezea mpira wa gofu?
Jibu ni kwamba, hela ndio chanzo ya hayo yote. Utafiti unaonesha kwamba wachezaji kama Ronaldo, Rooney na Neymar wanaweza kupata maelfu ya pauni kwa tweet moja tu kutoka kwa baadhi ya wadhamini wao wakubwa ulimwenguni. 
Orodha hii ya wachezaji wenye thamani kubwa katika mtandao wa Twitter, si tu kwa wanandinga bali pia hata kwa wachezaji wa michezo mingine kama vile staa wa NBA LeBron James na Kevin Durant ambao wote kwa pamoja wanaingia kwenye orodha hii.
Ronaldo inasemekana amejikusanyika kiasi cha pauni 169,280 kwa tweet yake dhidi ya bidhaa ya Nike.

Hii ndio orodha ya mastaa mbalimbali wa michezo ulimwenguni wanaoongoza kwa kunufaika na mtandao wa Twitter.
Arsenal playmaker Mesut Ozil recently retweeted a post by German sports brand adidas

NIGERIA ILIKUWA BADO KIDOGO TU WALIE TAIFA

$
0
0
Taifa Stars imelazimishwa sare ya bila kufungana dhidi ya Nigeria jioni ya jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar-es-salaam kwenye mchezo wa Kundi G wa kuwania kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2017.
Kwenye mchezo huo Stars ilionyesha kiwango kilichopitiliza ila tu ikashindwa kuzitumia nafasi ilizotengeneza.
Kwa upande wa Nigeria hawakuweza kutengeneza nafasi yoyote ya wazi kwenye dakika zote za mchezo. Mtetezi wao alikuwa golikipa Carl Ikeme, aliyeokoa michomo kadhaa ya washambuliaji wa Stars na kuufanya mchezo ubaki bila mabao.
Kikosi cha Taifa Stars kilionyesha kujiamini tangu dakika za mwanzoni za mchezo. Ni Thomas Ulimwengu aliyesumbua mno ngome ya Nigeria kupitia upande wa kulia kwenye dakika za mwanzo.
Mapema kwenye dakika ya 3 Ulimwengu alijaribu kumpita Kingsley Madu lakini mlinzi huyo wa Nigeria akamchezea madhambi na Stars wakatunukiwa Mpira wa adhabu ambao haukuweza kuzaa matunda yoyote.
Timu ziliendelea kushabuliana kwa zamu lakini Stars walionekana kuutawala mchezo zaidi. Kwenye dakika ya 21  Mrisho Ngassa alitishia kumpita Kenneth Omeruo lakini mlinzi huyo alimchezea madhambi na mwamuzi akaamuru mpira wa adhabu upigwe.
Mbwana Samatta alipiga mpira ule wa adhabu kwenye dakika ya 22. Shuti lake kali lililokuwa likielekea wavuni lilipanguliwa na golikipa Ikeme.

EDGAR DAVIDS KATIKA UBORA WAKE TENA, ATUPIA MBILI ZA HATARI DHIDI YA WAKONGWE WA MADRID JANA

$
0
0
Edgar Davids amerejesha kumbukumbu za miaka kadhaa nyuma baada ya kufunga magoli mawili kwa kukunjuka mashuti ya mbali (long range strikes) wakati wa pambano la ujirani mwema (charity) kati ya Laureus All Stars na wakongwe wa Real Madrid jana Jumamosi.
Kiungo huyo wa zamani wa Uholanzi huyo mwenye miaka 42 alifunga magoli hayo mawili kwa mashuti makali kutoka nje ya boksi.
Edgar Davids akishangilia baada ya kufunga moja kati ya magoli yake mawili ya hatari aliyofunga jana katika mechi dhidi ya Wakongwe wa Real Madrid.
Davids akiwa katika harakati za kumiliki mpira paembeni ya kiungo wa timu ya Wakongwe wa Real Madrid Claude Makelele (kushoto) wakati wa pambano lao lililopigwa jana.
Mfungaji bora wa muda wote wa Arsenal Thierry Henry naye pia alikuwa miongoni mwa wachezaji waliounda kikosi cha Laureus All Stars dhidi ya wakongwe wa Madrid.
Beki wa kulia wa zamani wa Brazil na AC Milan Cafu akipiga shuti kulelekea langoni mwa timu ya Wakongwe wa Madrid wakati wa pambano hilo lililopigwa katika dimba la AFAS Stadium.

Laureus waliifunga Madrid 6-5 katika pambano hilo lililolenga katika kuchangia mradi wa michezo kwa vijana waliopo Laureus huko Netherlands. 
Kwa kuanza na upande wa washindi, Davids alifunga mawili, kama ilivyo kwa staa wa zamani wa Celtic Pierre van Hooijdonk, huku nguli wa Arsenal Thierry Henry akifunga bao lake.
Kwa uapnde wa Real Madrid, magoli yao yalifungwa na Luis Figo, Ruben de la Red akipiga hat-trick na lingine likifungwa na Mholanzi Clarence Seedorf.
Clarence Seedorf (kushoto) akisubiri kurushwa kwa shilingi na akiwa na nahodha wa Wakongwe wa Madrid Fernando Hierro jana huko Alkmaar.
Clarence Seedorf .
Luis Figo naye alikuwepo kukipiga kwa upande wa Wakongwe wa Real Madrid.

MATOKEO YOTE YA MICHEZO YA JANA KUFUZU MATAIFA YA AFRIKA YAPO HAPA

$
0
0

FT
Liberia
Tunisia
FT
South Sudan
Equatorial Guinea
FT
Comoros
Uganda
FT
Botswana
Burkina Faso
FT
Guinea-Bissau
Congo
FT
Sao Tome and Principe
Morocco
FT
Tanzania
0 - 0
Nigeria
FT
Rwanda
Ghana
FT
Seychelles
Ethiopia
FT
Burundi
Niger
FT
Namibia
Senegal
FT
Mauritania
South Africa

YAPO HAPA MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JANA ZA KUFUZU MICHUANO YA MATAIFA ULAYA

CHUKUA FURSA YAKO KUANGALIA MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA KIRAFIKI ZILIZOPIGWA JANA

HII NDIO SABABU YA MEMPHIS KUTOKUTUMIA JINA LA BABA YAKE KWENYE JEZI YAKE

$
0
0
Namba saba: Memphis amechukua namba yenye heshima kubwa katika klabu ya Manchester United.
Baba yake Memphis Depay amemuomba mwanaye kumaliza tofauti zao ili kufungua ukurasa mpya wa maisha.
Nyota huyo wa Manchester United amekataa kutumia jina la ubini kwenye jezi yake kutokana na kutokuwa na maelewano mazuri na baba yake.
Memphis (21), mara zote amekuwa akisikika akisema kwamba baba yake alimtelekeza yeye na familia yake wakati akiwa na umri wa miaka minne.
Lakini baba yake, Dennis amekiri kosa hilo na kumuomba kijana wake amsamehe kwa yote yaliyotokea.
"Kusema kwamba sikumuona tena baada ya ile miaka minne ni uongo", aliliambia gazeti la the Sun."Ni kitu kisicho cha kawaida, sio vizuri. Yuke ni kijana wangu na nampenda sana. Mimi ndiye mtu wa kwanza kabisa kupatia mpira wake wa kwanza.
“Hakupewa matumzo mabaya na mimi. Hiyo si kweli.
“Nilimuona kupitia You Tube akiongea kuhusu baba yake, akisema kwamba hakutaka kuweka jina langu kwenye jezi yake. Ilinifanya nijisikie vibaya ana kwa kweli.
“Ningependa siku moja tuwe wote pamoja tena na kijana wangu. Namkumbuka sana kwa kweli”.

UNAMKUMBUKU RENE HIGUITA?, AFANYA KITUKO KINGINE CHA KUKUMBUKWA, INGIA HAPA KUJUA

$
0
0
Miaka ishirini imepita sasa tangu aliyekuwa mlinda mlango wa timu ya taifa ya Colombia Rene Higuita, apige tikitaka inayojulikana kwa jina maarufu la tikitaka ya Nge (scorpion kick) wakati akiokoa mpira uliokuwa unaelekea kuzama kimiani, katika mchezo dhidi ya England uliopigwa uwanja wa Wembley.
Sasa basi, Rene amerudia tena tukio hili, jionee mwenyewe hapo chini;
Na hii ndio ile aliyopiga miaka ishirini iliyopita;

KWELI VINCENT KOMPANY NI NOMA, AMCHEZEA RAFU HADI BINTI YAKE....(VIDEO)

$
0
0
Kuna tabia fulani ambazo humfanya Vincent Kompany kuwa moja ya mabeki wenye mioyo iliyojaa hali ya ushindani muda wote katika ligi kuu nchini Uingereza.
Mbelgiji huyo si tu kana kwamba yuko ngangari kwa muonekano bali tu, bali pia ni mkatili na mshindani pindi awapo uwanjani. Amezaliwa na chembechembe za ushindi ndani ya moyo wake ambapo wakati wote anaweza kufanya chochote ili mradi tu timu yake ipate matokeo.
Kwa nini yanasemwa maneno hayo, ni kutokana na kile alichokifanya kwa binti yake mwenye umri wa miaka 5 anayejulikana kwa jina la Sienna. Kompany alionekana akimkimbiza mwanae na wakat
i alipotaka kujifanya mjanja wa kukimbia, alimkwatua kidogo na kumuangusha chini bila ya kumletea maumivu yoyote yale.
Cheki video hapao chini;
/span>

SAMATTA AIGOMEA TP MAZEMBE

$
0
0
UWANJA wa Azam ambao ndiyo wa kisasa baada ya ule wa Taifa, Dar es Salaam ulijengwa kwa Sh 2 bilioni za Kitanzania hadi kuanza kutumika kwa mechi za Ligi Kuu Bara.
Lakini katika hali ya kushangaza Straika wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amegomea kiasi kama hicho cha fedha kujiunga na Zamalek ya Misri.
Katika kuonyesha jeuri zaidi, Samatta amesema pia hataongeza mkataba na klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, hata kama bosi wa timu hiyo Moise Katumbi atampa dau la maana kwa kuwa ndoto zake si kuendelea kucheza Afrika.
Samatta alisema ndoto zake kwa sasa ni kucheza soka la kulipwa Barani Ulaya na hawezi kuongeza mkataba wa kuichezea Mazembe, huku pia akikiri kuligomea dili la Zamalek ambalo lingempa Sh 2 bilioni.
Nyota huyo wa zamani wa Simba alikiri kuwa jitihada zake za kutimkia Ulaya mwaka huu tayari zimegonga mwamba, lakini hajakata tamaa na hataongeza mkataba Mazembe ili kujiongezea nafasi ya kujiunga na klabu za Ulaya.
“Dirisha limefungwa tayari kwa sasa, ila sijakata tamaa, nasubiri tena dirisha lijalo, mkataba wangu pia utakuwa unamalizika hivyo nitakuwa na nafasi kubwa zaidi,” alisema Samatta
“Kuhusu kuongeza mkataba Mazembe hapana, sina mpango huo, sina ndoto za kucheza tena Afrika na ndiyo sababu nilikataa dili la Zamalek hivi majuzi, sikupenda kujiunga nayo maana siyo ndoto yangu,” aliongeza.
Chanzo:Mwanaspoti

YANGA KUKUBALI HILI KWA MKWASA ISIPOKUWA UTARATIBU UFUATWE

$
0
0
YANGA kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Dk. Jonas Tiboroha, imesema wapo tayari kumwachia kocha msaidizi wao, Charles Boniface Mkwasa, kukitumikia kikosi cha timu ya Taifa, Taifa Stars, ikilitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufuata utaratibu.
TFF wapo katika mpango wa kumpa Mkwasa mkataba wa kudumu baada ya kuridhishwa na maendeleo ya Stars tangu kuondoka kwa Mholanzi, Mart Nooij, japo hajashinda mechi hata moja kati ya tatu walizocheza.
“Tupo tayari kumwachia, TFF wafuate utaratibu wa kuvunja mkataba, ana mkataba na sisi wa miaka miwili ambao ameutumikia kwa miezi minane tu,” alisema Tiboroha. 
TFF chini ya Rais Jamal Malinzi, walimteua Mkwasa kukaimu nafasi ya Kocha Mkuu wa Stars kwa muda wa miezi mitatu, muda ambao unaelekea kufikia ukingoni. 
Mkwasa alijikuta akizidi kujiongezea sifa baada ya wapenzi wa soka nchini kuishuhudia Stars ikicheza soka la hali ya juu dhidi ya Nigeria juzi na kutoka nayo suluhu.
Mchezo huo ulikuwa ni wa kuwania kufuzu fainali za Afrika (Afcon 2017) zitakazofanyika nchini Gabon.
Chanzo:Bingwa.

SABABU ZA WACHEZAJI WENGI WA KIAFRIKA KUTUMIA 'JUJU' HIZI HAPA

$
0
0
 Emmanuel Adebayor aliishutumu familia yake kumroga ili acheze chini ya kiwango.
Wachezaji wengi wa ngazi za juu wa Kiafrika wanaochezea ligi kuu Uingereza inasemekana wanaamini sana katika nguvu za giza kupata mafanikio katika soka.
Ripoti kutoka gazeti la the Sun zinadai kwamba wachezaji hao nyota wanaoamini katika hilo hutumia maelfu ya pauni kuwapa waganga wa kienyeji ili kuwapandisha viwango vyao
Wachezaji hao huenda kwa wapiga juju huko Afrika Magharibi, ambapo huoneshwa namna ya kufanya mambo ya miujiza ambayo pia husemekana kuondoa mikosi hasa ya majeraha ya mara kwa mara kwa wachezaji hao.
Mwanzoni kabisa mwa mwaka huu mchezaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor alimshuku mama yake kutumia nguvu za uchawi kumroga ili asiweze kupacika mabao pindi awapo uwanjani.

Hata hivyo, mshambuliaji wa zamani wa West Brom Brown Ideye amewaonya baadhi ya mastaa hao kwa kuamini katika nguvu hizo
Ideye alisema: “Nafahamu baadhi ya wachezaji ambao hutumia nguvu hizo lakini hawafanikiwi. Huu ni upuuzi tu. Wanaweza kupata mafanikio ya muda mfupi, lakini huwagharimu katika kipindi kirefu cha maisha yao. Waganga wana ushawishi mkubwa sana.
“Mara zote hawa ni watu ambao hujitahidi kujitafutia utajiri kwa njia zisizo halali kwa kukuambia uongo.
“Kama mambo kama haya yangekuwa yanafanyika, basi leo hii badala ya Messi na Ronaldo kuwa wanashinda kila siku uchezaji bora wa dunia, ingekuwa ni kwa wachezaji wa Kiafrika.
Baadhi ya uchawi hugharimu mpa Yuro 460 kwa mara moja.

JE, UNAKUBALIANA NA KAULI HII YA VICTORIA AZARENKA KUHUSU MESSI?

$
0
0
Nyota wa mchezo wa Tennis duniani Victoria Azarenka, amemimina pongezi kwa mchezaji mwenye kipaji cha ajabu ulimwenguni Lionel Messi, huku akisisitiza kwamba hucheza kama yupo kwenye 'video game' pindi awapo uwanjani.
Messi alifungia Argentina mabao mawili katika ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Bolivia Jumamosi wiki iliyopita, japokuwa bado hajafunga katika michezo miwili ya ufunguzi wa La Liga kwa timu yake mpaka sasa.
Mbelarusi huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye amefika robo fainali ya michuano ya US Open na kutoa shukrani zake za dhati kwa mashabiki baada ya ushindi wake dhidi ya Varvara Lepchenko, amesema kuwa uwezo wa nyota huyo wa Barcelona ni kitu kama "kisichofikirika"na kuongeza kuwa mara nyingi humwangalia wakati akiwa mapumzikoni.
"Kumwangalia Messi akicheza ni kama vile unaangalia video game", aliwaambai waandishi. "Ni kitu cha kusisimua sana.
"Nisingeweza kuangalia mchezo ule kwa sababu ya tofauti ya masaa na kwa sababu siku hizi nina majukumu mengi kidogo, lakini ningeweza kumwangalia kwa sababu ya umaridadi wake. 
"Anachokifanya Messi uwanjani ni kitu kisichoelezeka. Huwa najisikia furaha kubwa sana ninapomuangalia hasa akiwa na Barcelona na kusema tu ukweli, kwangu mimi, jamaa ni wa jabu sana. 
Azarenka alimalizia kwa kusema: "Wacheza soka hucheza kwa kutumia miguu. Siwezi kusema kwamba sidhani kama ubora wa mikono yangu katika Tennis ni kama yeye katika soka, lakini najaribu".
Viewing all 1447 articles
Browse latest View live