Kesho Jumamosi katika uwanja wa Mabatini , klabu ya Ruvu Shooting itachuana na Mtibwa Sugar katika mechi ya kirafiki.
Msemaji machachari wa Shooting, Masau Bwire amesema watatumia mchezo huo kunoa makali yatakayowapa ubabe kwa klabu za ligi daraja la kwanza msimu ujao.
Ruvu Shooting ilishuka daraja msimu uliopita sambamba na Polisi Morogoro, huku wakizipisha timu za Mwadui FC, Toto Africa, Maji Maji FC na African Sports.