"Mwaka huu kila mtu atakuwa anakimbia uwanjani vile mimi ninavyotaka, nitasema jinsi ninavyotaka vitu viende na wanatakiwa kusikiliza. Mchezaji pekee duniani ambae anaweza kucheza vile anavyotaka bila kufuata maelekezo yangu ni Leo Messi".
Unaweza kudhani maneno haya ni ya kocha wa Barcelona, Hapana! ni maeneno ya Pep Gurdiola akifanya mahojiano na na gazeti la Bild la Ujerumani akielezea mipango yake ya mwakani ya Bundesliga na michuano mingine ya Ulaya.
Baada ya hayo maneno makali, watu wengi wanaisubiri kwa hamu kuona jinsi gani Bayern ita-perform kwenye harakati zake hasa za kutetea ubingwa wake wa Bundesliga.
Pep alimaanisha kwamba mchezaji pekee ambae anaweza kucheza kwa kutumia ujuzi wake peke yake na kufanya kitu ambacho anakitaka au zaidi ya kile alichokitegemea.
