Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast kwa nyakati tofauti amefurahia maisha yake ya soka nchini England, Ufaransa, Uturuki na China, lakini mapokezi aliyoyapata jana katika klabu ya Montreal Impact ni noma sana.
Maelfu ya mashabiki walifika uwanja wa Ndege wa Pierre Elliott Trudeau kumpokea Drogba aliyejiunga na Montreal inayocheza ligi kuu ya Marekani.
![Hundreds of fans turned up at Pierre Elliott Trudeau International Airport to greet the Ivorian star]()

Drogba mwenye miaka 37 ameondoka Chelsea majira haya ya kiangazi baada ya kuichezea The Blues mechi 381 na kushinda makombe manne ya ligi kuu England katika vipindi viwili alivyokaa darajani.
"Hii ni siku kubwa sana katika histori ya klabu na kuwasili kwake kuna faida kubwa kwenye kila idara".
"Amekuwa kivutio kwa watu wengi tangu aanze kucheza soka na ataendelea kuwa na mvuto katika jezi zetu" Amesema Mkurugenzi wa ufundi wa Montreal, Adam Braz.
![The car carrying Drogba is mobbed by fans as he leaves the airport on Wednesday]()
