Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

OFFICIAL: YANGA YAMUUZA KPAH SHERMAN TIMU HII YA SAUZ

$
0
0
Mshambuliaji wa Yanga, raia wa Liberia, Kpah Sherman sasa maisha yamefikia kikomo Jangwani baada ya kuuzwa rasmi.
Katibu mkuu wa Yanga, Dr. Jonas Tiboroha amethibitisha kumuuza Sherman katika klabu ya Black Aces inayoshiriki ligi kuu soka nchini Afrika Kusini.
Hata hivyo, Tiboroha amesema dau walilomuuza straika huyo ni siri yao.
Sherman aliyeuzwa moja kwa moja anaondoka kwa ndege leo majira ya saa moja usiku kuelekea Bondeni kwa Madiba ambako anakwenda kuanza maisha mapya.
Nyota huyo aliyeshindwa kuwika Jangwani alisajiliwa wakati wa dirisha dogo mwezi Desemba mwaka jana.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles