Wanajeshi wa APR ya Rwanda wamefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya jirani zao wa LLB kutoka burundi.
Mechi nyingine Al Shandy ya Sudan kusini imeibuka kidedea kwa mabao 3-2 dhidi ya Hegeen ya Somalia.
Ushindi huo ni wa tatu kwa APR ambayo imezishinda Al Shandy, Heegen kabla ya kuimaliza LLB leo ndani ya uwanja wa Taifa, Dar es salaam.