Msimu wa 2013/14 , Luis Suarez na Daniel Sturridge walitikisa ligi kuu England wakikaribia kuchukua ubingwa wa ligi kuu England wakiichezea Liverpool, kabla ya Manchester City kuwapokonya tonge mdomoni.
Stori ni kwamba, tangu mshambuliaji aliyevuma Anfield, Fernando Torres aondoke Liverpool na kujiunga na Chelsea mwaka 2011 kwa paundi milioni 50, Luis Suarez ndiye mchezaji pekee aliyepata mafanikio.
Akaunti ya Twitter ya Tussen de lines ya Uholanzi leo imetengeeza Graphic ikionesha jinsi washambuliaji wa Liverpool walivyo na kiwango kibovu tangu Torres atimke kwa Majogoo.
Fabio Borini, Mario Balotelli, Andy Carroll, Robbie Keane, Iago Aspas na Rickie Lambert, wote wamekuwa wachovu katika suala la kucheka na nyavu.
Carroll, Borini, Balotelli na Keane wote wameigharimu Liverpool Euro milioni 4.8 kwa goli na takwimu zinaonesha kwamba David N’Gog angalau amejitahidi.
Graphic hii hapo chini inaonesha kiasi kilichotumika kumnunua kila straika na kuuzwa, idadi ya magoli na thamani ya kila goli.
