Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

OFFICIAL: PICHA 5 ZA UZI MPYA WA CHELSEA WATAKAOTINGA UGENINI MSIMU UJAO...

$
0
0
Rasmi: Chelsea leo wameachia picha za uzi mpya wa ugenini watakaotumia msimu ujao ukiwa na nembo ya mdhamini mpya.

Nyota wa klabu hiyo,  Eden Hazard, Nemanja Matic, Diego Costa, Gary Cahill na Thibaut Courtois wameonekana katika picha wakiwa wamevalia jezi hizo.

Mapema mwaka huu, Chelsea walitangaza kuingia mkataba na kampuni ya Yokohama Rubber Company ya Japan na kusaini mkataba wa miaka mitano ya udhamini wa jezi.

Kwa mujibu wa BBC, udhamini huo unaifanya Chelsea ivune paundi milioni 40 kwa mwaka ikimaanisha kwamba watachota paundi milioni 200 katika kipindi chote cha udhamini.

Udhamini huo wa Chelsea ni wa pili kuwa na thamani kubwa katika  historia ya soka la England, huku ule wa Manchester United wanaolipwa paundi milioni 53 kwa mwaka na Chevrolet ukiongoza.

Tazama picha zaidi za jezi mpya za Chelsea watazotumia ugenini....

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles