Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

AZAM WAWEKA MIKONO CHINI KWA TFF, BODI YA LIGI

$
0
0
Uongozi wa klabu ya Azam FC umeliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF )kuahirisha baadhi ya michezo yake ili ipate muda wa kuiandaa timu yao kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) dhidi ya Esperance ya Tunisia utakaopigwa Aprili 10 kwenye Uwanja Azam Complex, Chamazi.
Ofisa habari wa timu hiyo, Jaffar Idd aliwaambia wanahabari jijini Dar es Salaam kuwa kutokana na ugumu wa ratiba inayowakabili wanaiomba Bodi ya Ligi na TFF kuhairisha baadhi ya michezo yao ili kutoa nafasi ya wao kufanya maandalizi ya uhakika.
“Taarifa ya bodi (TPLB) inaonyesha Machi 31 tunatakiwa kucheza na Prisons ya Mbeya katika mchezo wa Kombe la FA, pia mchezo wetu na Toto Africans ya Mwanza ambao ilibidi uchezwe Aprili 4 umerudishwa nyuma hadi Aprili 3, ratiba hii inatubana kwa kweli, tunaiomba bodi ya ligi na TFF itusaidie,” alisema.

Hata hivyo, mkurugenzi wa bodi hiyo, Boniface Wambura alipotafutwa kuzungumzia suala hilo alisema wanayafanyia kazi maombi ya Azam.
Katika hatua nyingine, waamuzi watakaochezesha mchezo kati ya Azam na Esperance wanatoka Afrika Kusini na watawasili siku moja kabla ya mchezo huo, ilieleza TFF.
Credit:Bongosoka.com

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles