
Mshambulizi wa Tottenham na England Harry Kane ameweka tageti zake za kufunga ili kumfikia Leo Messi.
Akiwa na magoli 30 kwa klabu yake na timu yake ya taifa msimu huu, Kane ameibuka kuwa moja ya washambuliaji wenye ubora wa hali ya juu kunako Ligi kuu Uingereza.
Akiwa bado na safari ndefu ya kumfikia mshambuliaji wa Argentina na Barcelona, Kane bado hajakata tamaa kabisa.
Kane anatakiwa kufunga mabao 21 dhidi ya Norwich wikiendi hii ili kufikia rekodi ya Messi ya mwaka huu wa 2015, hivyo ameamua kufanya masihara katika akaunti yake ya Twitter kwamba anaenda kufanya maajabu ili kufukia rekodi hiyo.