Guus Hiddink amesisitiza kuwa Chelsea wanaweza kubadili kabisa matokeo mabaya yanayowakumba msimu huu na punde tu baada ya kutangazwa kocha mkuu wa klabu hiyo akirithi mikoba ya Mreno Jose Mourinho.
Mdachi huyo alikuwa jukwaani akishuhudia Chelsea wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 3-1 dhidi ya Sunderland jana, huku Steve Holland na Eddie Newton wakishikilia wakikiongoza kikosi hicho kwa muda.
Hiddink alifurahia maisha klabuni hapo wakati alipokuwa kocha wa muda baada ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo Mbrazil Luiz Felipe Scolari kufukuzwa mwaka 2009 na kusema kusisitiza kuwa anasubiri kwa hamu fursa ya kukinoa kikosi hicho kwa mara nyingine tena.
"Nimefurahi sana kureje klabuni hapa," aliiambai tovuti ya klabu. "Chelsea ni moja ya vilabu vikubwa duniani na haipasi kuwa hapa ilipo kwa sasa.
"Hata hivyo nitahakikisha kuwa tunabadili kila kitu na kureje katika hali ya kawaida," alisema