Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

WATU KUMI AMBAO INAWEZEKANA WAMEFURAHISHWA NA KUFUKUZWA KWA MOURINHO

$
0
0
Mashabiki wengi wa soka ulimwenguni wameshtushwa n kusikitishwa na taarifa za kufukuzwa kwa Jose Mourinho.
Kwa mashabiki wa timu tofauti tofauti, taarifa ya za kufukuzwa kwa 'The Special One' kutaacha pengo kubwa sana kwenye 'Premier League' hasa kutokana na aina ya vituko alivyokuwa navyo Mourinho na kuifanya Ligi Kuu England kuwa na msisimko wa aina yake.
Hawa ndio watu 10 ambao kufukuzwa kwa Mourinho kamwe hakutawashtua kwa namna yoyote ile;

Lionel Messi.
“Unazungumziaje suala la udanganyifu huko Katalunya ?”
“Je Messi anaweza kufungiwa kwa kudanganya? Barcelona ni jiji la asili lenye 'theatres' nyingi sana na kijana huyu amejifunza vizuri sana. Amejifunza namna ya kudanganya vizuri sana.
Baada ya beki wake wa kushoto Asier Del Horno kutolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Messi wakati wa pambano la Ligi ya Mabingwa mwaka 2005/06.

Cristiano Ronaldo
"Kwa mara ya kwanza kabisa nilikuwa kocha mwaka 2000 lakini, kabla ya hapo, nilikuwa kocha msaidizi wa timu kubwa na makocha wakubwa na kuwafundisha wachezaji wakubwa. Nikiwa na umri wa miaka nimemfundisha Ronaldo - lakin i sio huyu [Cristiano], yule halisi, Ronaldo wa Brazil."

Arsene Wenger
“Nadhani ni moja ya watu ambao ni wa jabu sana ambao hupenda kuona sehemu za siri za wenzao (voyeur). Anapenda kuangalia wenzake. Kuna baadhi ya watu ambao, wanapokuwa nyumbani, wana hadubini kubwa ambayo kazi yake kubwa ni kuangalia kinachotendekea katika familia za watu. Anaongea ongea tu kuhusu Chelsea.”
Hii ilikuwa ni mwaka 2015

Kocha wa zamani wa Newcastle John Carver
"Unaweza kuweka ng'ombe katikati ya uwanja. Halafu usimamisha mchezo kwa sababu kuna ng'ombe. Huwezi kujifanyia chochote tu kwenye mchezo wa mpira wa miguu. Unatakiwa ulinde kwa kutumia wachezaji 10, weka wachezaji hao 10 katikati ya goli, halafu paki basi, lakini mchezo wa mpira wa miguu huhitaji mpira." Kauli ya Mourinho kwa Carver baada ya kufungwa na Newcastle.

Pep Guardiola
"Guardiola ni kocha wa aina yake lakini nimeshinda maombe mawili ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. yeye ameshinda moja tu na hicho ndicho kitu ambacho pengine kingenisumbua sana. Ningekuwa najisikia aibu sana kushinda kwa skendo ya Stamford Bridge na akishinda tena mwaka huu itakuwa ni skendo ya Bernabéu.

Didier Drogba
"Kwa sasa sio tena kocha wa Chelsea, na siwezi kuwatetea tena, lakini nadhani ni sahihi kama nikisema Drogba ni mtu wa kujiangusha (diver)."

Rafa Benitez
"Nilidhani angenishukuru kwa kumpa ubingwa. Waulize mashabiki wote wa Inter juu ya wanachofikiri kati yangu na yeye."
Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Jose kumkejeli Rafa - na haikuwa mara ya mwisho tena. Jose anajibu mapigo baada ya Inter kubeba ndoo ya 'Club World' mwaka 2010 ikiwa ni miezi michache tu baada ya kuondoka klabuni hapo.

Claudio Ranieri
“Ni mzee na hajashinda chochote kile. Nilisoma Kiitalaino masaa matano kwa siku kwa miezi mingi kuhakikisha ningeweza kuwasiliana vizuri na wachezaji, vyobo vya habari. Ranieri amekaa Uingereza kwa takribani miaka mitano lakini bado alishindwa kusema hata ‘good morning’ na ‘good afternoon.'"
Kwa sasa hakuna uhusiano muri kati ya wawili hao.

Carlo Ancelotti
“Makocha wengi sana wameshinda zaidi ya mara moja lakin i kuna klabu moja tu ambayo ilikuwa ikiongoza kwa mabao 3-0 wakati wa fainali na wakapoteza mchezo huo.”
Mourinho alitoa kauli hii kwa Ancelotti

Mrs. Benitez
“Kama atautumia vizuri muda wake kumfanyia mume wake mlo kamili basi sidhani kama atakuwa na nafasi yoyote ya kuongea kuhusu mimi."
Mourinho alimjibu mke wa Rafa Benitez.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles