Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

SHAWCROSS AMKEJELI COSTA

$
0
0
Mlinzi wa kati wa Stoke City Ryan Shawcross amesema kuwa, Diego Costa alifanya kosa kubwa sana kutumia muda mwingi kutaka malumbano uwanjani badala ya kucheza mpira zaidi, kwenye mchezo ambao Chelsea walipoteza kwa kufungwa goli 1-0 mwishoni mwa wiki iliyopita.
Wawili hao walikuwa na malumbano kwa takriban muda wote wa mchezo, lakini alikuwa ni Shawcross ambaye alibaki na kicheko baada ya timu yake kuibuka na ushindi kwa goli pekee lililowekwa kimiani na Marko Arnautovic.
Costa amekuwa na tabia ya kuwafanyia vurugu mabeki wa timu pinzani, lakini Shawcross amesema yeye hakuwa akijihusisha kabisa na mshambuliaji huyo.
" Costa alikuwa akihangaika na mimi na sio kucheza mpira, kilichotokea ni kwamba mimi ndio nimeibuka mshindi,"alisema wakati wa mkutano wa Jukwaa la mashabiki Jumatano wiki hii.
"Costa ni mchezaji wa kiwango cha juu na nimefarijika sana kumfunga mdomo."

Viewing all articles
Browse latest Browse all 1447

Trending Articles