Chelsea wamethibitisha kumsajili mshambuliji wa Kolombia Radamel Falcao kwa mkopo wa msimu mzima kutoka klabu ya Monaco.
Falcao,29, msimu uliopita alikipiga kwa mkopo kwa mashetani Wekundu klabu ya Manchester United, na kufanikiwa kufunga magoli manne tu katika michezo 29 aliyocheza.
"Nina furaha kubwa kujiunga na Chelsea na nasubiri kwa hamu kuanza mazoezi na wenzangu ili tuweze kulitetea taji la ligi kuu na pia kupata mafanikio katika michuano ya Ulaya," Falcao aliiambia tovuti ya Chelsea.
Falcao pia amewahi kuzichezea timu za River Plate, Porto na Atletico Madrid.