Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all 1447 articles
Browse latest View live

LEHMANN AZUNGUMZA KAULI HII DHDI YA CECH KUFUATIA KURUHUSU MAGOLI YA KIZEMBE DHIDI YA WEST HAM

$
0
0
Nguli wa Arsenal Jens Lehmann amemsisitiza Petr Cech kufurahia msimu bora kabisa katika klabu ya Arsenal, lakini amemuasa kuwa anahitaji muda kuweza kuzoea maisha mapya klabuni hapo kufuatia uhamisho wake kutoka Chelsea.
Cech alifanya makosa ya kizembe ambayo yaliigharimu Arsenal kupoteza mchezo wake wa kwanza wa ligi kwa mabao 2-0 dhidi ya West Ham uliopigwa Jumapili katika dimba la Emirates huku ukiwa ndio mchezo wake kwanza wa ligi akiwa ndani ya uzi wa Arsenal.
Lehmann, ambaye alikuwa katikati ya lango katika kikosi cha Arsenal kilichotwaa ndoo ya EPL bila ya kufungwa msimu wa 2004, amekiri kushtushwa na kiwango cha Cech lakini anaamini kwamba mlinda mlango huyo atakuja kivingine na kuonesha yale aliyokuwa akiyafanya pindi alipokuwa Chelsea.
"Nimeshangazwa kwa sababu nilitarajia kuona akionesha kiwango kikubwa punde tu msimu unapoanza”, Lehmann alikaririwa na mtandao wa Goal kutoka Marekani.
"Lakini wakati mwingine inachua muda kidogo kuzoea mazingira mapya, hasa unapotoka kwa mahasimu wako wakubwa kama Chelsea. Huchukua muda kwa kweli, cha msingi anatakiwa kusahau yote hayo.


"Ni aina ya makipa ambao Arsenal walikuwa wakihitaji ili kutwaa ubingwa", Lehmann aliongeza. "Ana uzoefu wa kutosha, yaani ana sifa zote za kuwa mlinda mlango bora na naweza kusema ni miongoni mwa walinda mlango bora kabisa ulimwenguni.

UNAJUA KUWA NI BEKI GANI AMBAYE NEYMAR HUMUHOFIA ZAIDI UWANJANI, MWENYEWE AMEMTAJA HAPA

$
0
0
Neymar reveals the toughest defenders and best goal of his career
Neymar amemtaja Sergio Ramos kuwa ni moja ya mabeki visiki kabisa aliowahi kukutana nao katika maisha yake ya soka.
Nyota huyo wa Barcelona amemuelezea mlinzi huyo wa kati wa Real Madrid kama " beki kisiki" wakati alipokuwa akiulizwa ni beki gani ambaye anahisi humletea shida katika maisha yake ya soka.
Lakini hata hivyo Neymar pia amesema wachezaji wenzake Javier Mascherano na Gerard Pique pia humpa shida wakati wakiwa mazoezini bila ya kusahau Mbrazil mwenzake Thiago Silva.
"Ni vigumu kusema kuhusu hili, kuna mabeki wengi sana wa kiwango cha juu" alisema. "wapo kina Mascherano, Pique, Thiago Silva ila Sergio Ramos - ni beki wa kati bora sana".

TORRES AMPA MANENO MATAMU PEDRO JUU YA UHAMISHO WAKE KUELEKEA UNITED

$
0
0
Fernando Torres amezidi kumpa nguvu Mhisapaniola mwenzake Pedro, kuwa atapata mafanikio makubwa endapo ataelekea kucheza ligi kuu nchini Uingereza.
Hali hiyo imetokana na tetesi kuwa Pedro yuko mbioni kujiunga na Manchester United akitokea klabu ya Barcelona, huku fununu nyingine zikieleza kuwa tayari miamba hiyo imeshafikia makubaliano ya ada ya mwanzo ya uhamisho ya pauni milioni18.1 na nyongeza(bonus) ya pauni milioni 4.2 endapo mchezaji huyo atafanya mambo makubwa zaidi.
Torres, ambaye amecheza EPL kwa takribani miaka 7 akiwa na Liverpoo na baadaye Chelsea, amesisitiza kuwa Pedro ana uwezo wa kucheza England hasa ikizingatiwa anataka nafasi zaidi ya kucheza.
“Ni rafiki yangu sana, na endapo ataamua kuelekea Uingereza, basi naamini atafanya vizuri tu”. Torres aliliambia Daily Mirror.
“Ana sifa zote za kukipiga EPL, amekuwa Barcelona kwa miaka mingi sana, hivyo naamini ana uwezo mkubwa ukiongezea pia na nidhamu ya uwajibikaji wake uwanjani.

ACHANA NA TUKIO LA EVA CARNEIRO, HAYA NDIO MATUKIO MENGINE YALIYOMHUSISHA MOURINHO NA TIMU YAKE YA MADAKTARI

$
0
0
Uhusiano wa Eva Carneiro na Jose Mourinho umeingia dosari baada ya kocha huyo Mreno kumuondoa katika idara ya tiba itakayokuwa inasafiri na timu katika michezo mbalimbali na hata pia mazoezini.
Mourinho aliikosoa hadharani idara takje ya tiba baada ya sare ya mabao 2-2 dhdi ya Swansea City, kutokana na kwenda kumtibu Hazard, hali ya kuwa Mourinho anadai kiungo huyo alikuwa hajapata maumvivu yoyote, huku timu yake ikizidi kubaki pungufu, baada ya mlinda mlango wake Thibaut Courtois kutolewa nje kwa kadi nyekundu.
Lakini kumbukumbu ziandai kuwa hii si mara ya kwanza kwa Mourinho kufanya tukio hili.
Eva Carneiro akirushiana maneno na Jose Mourinho 

Februari 2005: Daktari wa Chelsea Neil Frazer aliondoka.
Ukiwa ni mwezi mmoja tangu Mourinho ajiunge na Chelsea kwa mara ya kwanza akaanza mzozo na timu yake ya madaktari baada ya kusababisha winga wake wakati huo Arjen Robben kukumbwa na majeraha ya mara kwa mara
Neil Frazer aliamua kuondoka wiki kadhaa kabla ya pambano la fainali ya kombe la Carling dhidi Liverpool baada ya kutoa taarifa kuwa Robben angekuwepo katika mchezo dhidi ya Cardiff huku winga huyo akiwa ametoka kuvunjika mguu takaribani wiki tatu nyuma.
Kutokana na taarifa hiyo, inasemekana Daktari huyo alitimuliwa siku chache baada ya tukio hilo, ingawa Chelsea walikanusha na kusema kuwa, ameamua kuondoka kutokana na matatizo ya kiafya yaliyokuwa yakimsumbua.
Arjen Robben akiwa chini kuugulia jereha lake la mguu.


October 2006: Jeraha la kichwa la Petr Cech dhidi ya Reading
Mourinho alitoa kauli hii: 'Endapo kipa wangu atakufa katika vyumba vya kubadilishia nguo aku akiwa njiani kuelekea hospitali Chama cha Mpira cha Uingereza lazima wafikiri mara mbili mbili'.



Novemba 2014: Mourinho amjia juu Sergio Ramos 
Hii ilikuwa ni baada ya Sergio Ramos kutilia shaka uamuzi wa Mourinho kukataa kuwaruhusu Diego Costa na Cesc Fabregas kujiunga na timu yao ya taifa.
Mourinho akasema hivi;'Tangu nimemfahamu Sergio Ramos amekuwa ni mchezaji wa aina ya kipekee sana, lakini sio daktari,' alisema. 'Sio yeye wala mimi ambaye ni daktari. Nafanya kila liwezekanalo ila mimi sio daktari.
Lakini cha kushangaza Costa alicheza mchezo dhidi ya West Brow ilhali ilisemekana kuwa ni mgonjwa.



May 2015: Chelsea walikosolewa dhdi ya jeraha la kichwa la Oscar.
Hii ilitokan na wataalamu kusema kuwa haikuwa sahihi Oscar kurudi uwanjani baada ya kugongana na kipa wa Arsenal David Ospina lakini, Mourinho kwa upande wake akasema kuwa Oscar hakuwa na maumivu yoyote hivyo yalikuwa yakiongelewa yoyote yalikuwa ni uongo.

TP MAZEMBE, MAMELODI SUNDOWNS KUTUA TANZANIA KUCHEZA MASHINDANO

$
0
0
Timu za TP Mazembe ya Congo DRC na Mamelodi Sundowns ya nchini Afrika Kusini zinatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ajili ya kucheza mashindano maalumu ya kumuaga Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete anayemaliza muda muda wake madarakani kama Rais mwezi Octoba mwaka huu.
Klabu hizo zitaongozana na wamiliki wake ambapo Moise Katumbi ataongozana na klabu yake ya TP Mazembe kwenye safari hiyo ya kuja Tanzania wakati Patrice Motsepe nae atakuja pamoja na timu yakeya Mamelodi Sundowns kuja kumuaga Rais Kikwete katika mashindano hayo maalumu .
Kwa upande wa Tanzania, timu mbili zitakazothibitisha mapema ushiriki wake kati ya Azaim FC, Yanga SC na Simba SC zitapata fursa ya kushiriki mashindano hayo maalumu  ya kumuaga Dkt. Jakaya Kikwete ambayo yatashirikisha timu nne mbili zikiwa ni TP Mazembe na Mamelodi Sundowns na timu mbili za Tanzania.
Rais Kikwete anafahamika kwa kuwa miongoni mwa marais wa Tanzania ambao wanapenda michezo na amesaidia kwa kiasi kikubwa kukua na kuendelea kwa michezo nchini husunan soka katika kipindi chote ambacho amekuwa madarakani.
Endele kufuatilia mtandao huu tunaendelea kutafuta tarehe na siku ambayo mashindano hayo maalumu yatafanyika ikiwa ni pamoja na ratiba nzima ya mashindano hayo pindi tutakapopata taarifa rasmi tutakujuza kila kitu.

SIMON MSUVA AWATAHADHARISHA MASTRAIKA YANGA

$
0
0
MFUNGAJI Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Simon Msuva, amewataka washambuliaji wenzake wa Yanga, akiwamo Mzimbabwe Donald Ngoma, kutotegemea mteremko kupata heshima ndani ya klabu hiyo, akiwasisitizia kupambana vilivyo.
Mbali ya Ngoma, Yanga imesajili straika wapya watano wengine wakiwa ni Deus Kaseke, Malimi Busungu, Geoff rey Mwashiuya na Matheo Simon ambao wanaungana na wale wa zamani kuunda safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.
Akizungumza na BINGWA kutoka Mbeya jana, Msuva alisema kuwa binafsi amejiandaa vizuri kuendeleza makali yake kama mfungaji na mchezaji bora wa msimu uliopita, akikiri kukabiliwa na ushindani mkubwa wa namba katika kikosi chao.
“Ni kweli kuna ushindani mkubwa wa namba lakini hilo si tatizo kwangu kwani inategemea na utendaji kazi wangu, nitaweka bidii ili niweze
kupata namba katika kikosi cha kwanza,” alisema.

CHEKI MAKAMUZI YA YANGA HUKO TUKUYU....

$
0
0
 Mabingwa wa kandanda Tanzania bara, Dar es salaam Young Africans wanaendelea na mazoezi mjini Tukuyu, Mbeya kujiwinda na mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC itayopigwa Agosti 22 mwaka huu uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Wakiwa huko, Yanga tayari wamecheza mechi mbili za kirafiki ambapo ya kwanza walishinda 4-1 dhidi ya Kimondo FC.
Magoli ya Wanajangwani katika mchezo huo uliopigwa uwanja wa CCM Vwawa Mbozi yalifungwa na Geofrey Mwashiuya (mawili), Simon Msuva na Amissi Tambwe.
Yanga jana imecheza mechi nyingine dhidi ya Tanzania Prisons uwanja wa Sokoine ambapo ilishinda 2-0, magoli yakifungwa na Malimi Busungu na Amissi Tambwe.
Jumapili ya wiki hii, Yanga watakabiliana na Mbeya City uwanja huo wa Sokoine.



VIDEO: BAADA YA KUPIGANA NA AFANDE, SASA PAULO WANCHOPE AFIKIA MAAMUZI HAYA...

$
0
0
Meneja wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Costa Rica, Paulo Wanchope amebwaga manyanga siku moja baada ya kuhusika na tukio la kupigana wakati wa mchezo huko Panama.
Paulo Wanchope mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Costa Rica aliyewahi pia kucheza ligi kuu nchini Uingereza katika timu za Derby County na Manchester City alikuwa akitazama timu yake ya taifa ya vijana walio chini ya miaka (23) wakati vurumai hizo zikizuka.
Paulo anaonekana katika mkanda wa video akiwa na hasira huku akifungua geti karibu na uwanja ambapo alianza kupambana na bwana mmoja kabla ya wanausalama kuingilia kati.
Vyombo vya habari nchini humo vimesema kuwa meneja huyo hakua na furaha na muamuzi wa mchezo huo,pamoja na hayo mchezo huo uliisha kwa matokeo ya bila kufungana.


MREMBO HUYU AKUBALI ADHABU YOYOTE ILE KAMA BENZEMA HATATUA KLABU HII

$
0
0
Mwanamitindo wa Venezuela, Jeinny Lizarazo ameendelea kugonga vichwa vya habari barani Ulaya.
Mapema wiki hii alidai kwamba Arsenal wanakaribia kukamilisha usajili wa nyota wa Real Madrid, Karim Benzema, lakini mpaka sasa haijatokea.

Lizarazo alifafanua kwamba Benzema anaelekea kuchukua vipimo vya afya Emirates.
Leo mrembo huyo amewapoza mashabiki wa Arsenal akisisitiza kwamba lazima dili hilo litokee, huku akifika mbali zaidi kwa kusema kwamba, kama taarifa yake sio sahihi mpaka Agosti 29 mwaka huu,  yuko tayari  kupata adhabu yoyote ile.
Tunza tarehe hii kwenye kitabu chako...manake kakubali adhabu yoyote unayoona safi.....

NIMEKUWEKEA HAPA WATU 10 MAARUFU DUNIANI AMBAO WANASEMA CHRISTIANO RONALDO NDIYE NYOTA WA DUNIA

$
0
0
1. Jose Mourinho 
‘‘Cristiano Ronaldo ni mtambo wa magoli. Ni bora na kamwe hakutakuja kutokea Ronaldo mwingine’’ Jose Mourinho

2. Fernando Torres 
‘‘Kwa upande wangu Cristiano Ronaldo ni mchezaji bora ulimwenguni. Ni mtambo wa mabo usiofananishwa na mtu yeyote yule’’ Fernando Torres.

3. Bobby Charlton
‘‘Anafanya vitu ambavyo sijawahi kuvishuhudia hapo awali kwa mchezaji mwigine yeyote na kiukweli ni lazima upatwe na mshangao mkubwa sana pale unapomuangalia’’, Sir Bobby Charlton.

4. Rio Ferdinand
‘‘Angeweza kuwa mchezaji mkubwa sana lakini anaelekea kuwa mchezaji bora kabisa duniani, na sasa ndivyo alivyo’’, Rio Ferdinand.

5. Lee Clayton 
‘‘Nguvu, kasi. Boksi la ofisi ya mpira. Naweza kusema huyu ni George Best bila shaka’’ Lee Clayton

6. Carlos Queiroz 
Atakuja kuwa nyota wa dunia kama Michael Jordan katika mchezo wa mpira wa kikapu. Wote kwa pamoja wamebarikiwa akili ambazo haziwahi kuonekana hapo kabla’’, Carlos Queiroz.

7. Liam Payne – One Direction star
‘‘Cristiano Ronaldo ni mchezaji anayenivutia. Ni mchezaji bora ulimwenguni’’, nyota wa One direction Liam Payne.

8. Sir Alex Ferguson 
‘‘Tumekuwa na baadhi ya wachezaji wakubwa sana hapa klabuni kwa miaka takribani 20, lakini huyu ni zaidi ya wote hao’’, Sir Alex Ferguson.

9. George Best 
“Kumekuwa na wachezaji wachache sana ambao wamekuwa wakiitwa kama George Best wapya kwa miaka mingi tu, lakini hii ni mara ya kwanza kwangu kukubaliana na kauli hii”, George Best.

10. Cesc Fabregas 
“Kwangu mimi, ni mchezaji wa kipekee.” Cesc fabregas

TWEET YA NYOTA HUYU WA MANCHESTER UNITED YAMALIZA KILA KITU.....

$
0
0
Wiki za karibuni kumekuwepo na tetesi nyingi zinazomuhusisha Winga kinda wa Manchester United,  Adnan Januzaj kujiunga na klabu ya Sunderland.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye miaka 20, leo amekanusha tetesi hizo kwa tweet ya neno moja tu ambalo linaashiria haendi popote majira haya ya kiangazi.
Januzaj alianza katika mechi saba tu msimu uliopita chini ya Louis van Gaal, lakini alitumika pia katika maandalizi ya msimu mpya ambao tayari umeanza kutimua vumbi.
Sunderland ambao walifungwa 4-2 na Leicester City katika mechi ya ufunguzi wa ligi kuu ya England mwishoni mwa Juma lililopita bado wanatafuta wachezaji wapya.
Adnan Januzaj hakupangwa kabisa katika kikosi cha Manchester United kilichocheza mechi ya ufunguzi dhidi ya Tottenham na kuibua tetesi kuwa anakwenda Sunderland kwa mkopo.
Hata hivyo, Tweet yake ya leo inamaanisha hakuna dili la kutua kwa paka hao weusi.



CHEKI MIUJIZA YA WATOTO HUKO ENGLAND, BILA SHAKA HUJAWAHI KUONA AISEE!...

$
0
0
Siku za karibuni Darren Urquhart na Tom Smith wameanzisha project moja ambayo wameipa jina la “Bad Boys FC”.
Wawili hao wamekumbushia  baadhi ya matukio makali yaliyowahi kutokea katika ulimwengu wa soka ambapo wamewahusisha watoto.
Project hiyo imetumia baadhi ya picha zisizosahaulika katika mchezo wa soka.

Urquhart na Smith walieleza kwamba, wameamua kufanya hivyo ili kuona kama wanamichezo wa sasa wanaweza kuigwa na vijana katika soka la England, wakati huu kuna mishahara mikubwa na maisha mazuri kwa mastaa wa kandanda.
Hapa chini ni picha kutoka project ya  Bad Boy FC 
1. Why Always Me – Mario Balotelli.
Hii haitasahaulika na hapa wamewahusisha watoto ambao wameigiza tukio hilo, huku mmoja akiigiza kama nyota wa Manchester United,  Anderson na  Man City,  David Silva.
Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)
2. Tiny Hand of God – Diego Maradona
Hili ni goli la Mkono wa Mungu alilowahi kufunga Diego Maradona, hakika watoto kwa asilimia mia wameigiza kuanzia namna alivyoweka miguu.
Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)
3. Baby Teeth – Luis Suarez
Tukio hili la Luis Suarez kumng'ata  Branislav Ivanovic nalo wamejitahidi kuliigiza hapa chini;
Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)
4. Kicking & Screaming – David Beckham
Tukio hili ambalo lilifanywa na  Beckham nalo limeigizwa na watoto
Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)
5. My Mum’s a What?! – Zinedine Zidane
Hili ni tukio alilofanya Zidane dhidi Marco Materazzi wa Italia.
Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)
6. Karate Kid – Eric Cantona
Cantona aliwahi kumshambulia shabiki kwa Kareti, huku mwanamke mmoja kulia akionekana kushangaa. Hapa wamejitahidi kukumbushia tukio hilo.
Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)
7. Learn to Play Nice- Martin Keown
Hili ni tukio la Keown na Ruud van Nistelrooy 
Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)Kids recreate famous footy moments ft. Suarezs bite v Chelsea, Cantonas kung fu kick (Pictures)

OFFICIAL: ARSENAL WAZINDUA JEZI MPYA YA TATU MSIMU HUU, UNAIPA MAKSI NGAPI?

$
0
0
Arsenal leo wamezindua jezi yao mpya ya tatu watakayotumia msimu wa 2015/2016.
Uzi huo uliotengenezwa na PUMA utavaliwa na timu ya kwanza katika mechi za ugenini za makombe ikiwemo Uefa Champions League ambayo itaanza mwezi Septemba.
Jezi hii ni ya  mwisho kwa Arsenal kwa msimu huu, kwani mwezi Juni na Julai mwaka huu walianika jezi za nyumbani na ugenini.
Tazama picha ya jezi mpya  ya Arsenal (juu na chini)
Its Official: Arsenal unveil their brand new 3rd kit for the 2015 16 season (Pictures)
Its Official: Arsenal unveil their brand new 3rd kit for the 2015 16 season (Pictures)
Its Official: Arsenal unveil their brand new 3rd kit for the 2015 16 season (Pictures)

Its Official: Arsenal unveil their brand new 3rd kit for the 2015 16 season (Pictures)

UGOMVI WA MOURINHO NA DAKTARI WAKE WAIBUA HISIA ZA UBAGUZI WA KIJINSIA

$
0
0
Daktari wa timu ya Chelsea, mwanadada Eva Carneiro wiki hii amepigwa stop kuendelea kukaa katika benchi la timu hiyo na mazoezini kwa ujumla, kutokana na kutokuelewana na meneja wa klabu hiyo Jose Mourinho.
Katika tukio lililotokea wikend iliyopita Chelsea wakitoa sare ya 2-2 na Swansea katika uwanja wa Stamford Bridge, Mourinho katika hali isiyo ya kawaida, alimbwatukia daktari huyo mwanamke kwa kile alichosema, daktari huyo alichelewesha muda wakati timu yao inahitaji matokeo kwa kwenda kumtibu Eden Hazard ambaye Mourinho anaamini hakuumia bali alikua kachoka.
Kauli hizi za Mourinho zimewashangaza wengi na kuwakera wengi wa mashabiki wa klabu hiyo kwa kumuona Mourinho amekosa busara na heshima mbele ya taaluma ya dada huyo aliyekaa klabuni hapo tangu mwaka 2009.
Penye wengi, pana mengi pia. Kupitia katika mitandao ya kijamii, mashabiki mbalimbali ulimwenguni kote waliandika hisia zao kutokana na sakata hilo. Lakini kama ilivyo kawaida, penye wengi, wapo waliomtusi kocha wao Jose Mourinho, lakini hawakukosa waliomdhihaki mwanadada huyo kwa kuhusisha utendaji kazi wake na jinsia yake.

Juzi, daktari huyo aliandika kupitia ukurasa wake wa Facebook, kuwashukuru mashabiki duniani kote kwa meseji za faraja katika wakati huu mgumu kwake.
Eva, amefungiwa kukaa katika benchi wala kuhudhuria mazoezi ya timu yake na kocha Jose Mourinho raia wa Ureno, ingawa ataendelea wazifa wake wa kuwa daktari namba moja wa timu.
Eva Carneiro received the brunt of Mourinho's criticism after rushing on to treat Eden Hazard's injury
Wachambuzi wa mambo ya jinsia nchini England, wanahusisha tukio hili na lile lililokuwa kati ya kocha huyo huyo Mourinho walipozozana na mke wa kocha wa Real Madrid, Rafael Benitez wiki iliyopita, baada ya Jose Mourinho kumkashifu Benitez kuwa ana kitambi.
Katika ugomvi huo na mke wa Benitez, Mourinho alimtaka mwanamke huyo kuacha kuingilia mambo yasiyo muhusu na badala yake akamkashifu kwa kumtaka akae nyumbani na kumuandalia chakula mumewe.
Matukio haya yote mawili kati ya Mourinho na wanawake hawa yanaleta tafakari ya ubaguzi wa kijiinsia 'sexism' ambao Mourinho kauanzisha katika soka.
Kwanini lakini haya yote? Mourinho anasema alikasirishwa na kitendo cha daktari huyo kuingia uwanjani kumtibia Eden Hazard kwa anachokiamini Mourinho kwamba Hazard alikua kachoka. Lakini mikanda ya kipande hicho yanaonesha kwamba daktari huyo aliitwa na mwamuzi akafanye kazi yake.

Wachambuzi wengi wanaamini Mourinho yuko katika wakati mgumu 'stress' kutokana na kutofanya usajili mzuri huku akitakiwa kutetea ubingwa wa ligi hiyo ya nchini England, sanjari na kufanya vizuri katika michuano mingine, huku timu yake ikionekana kutokuwa imara.
Makocha wengi wamekuwa wagumu kuweka ukweli hadharani na badala yake, wamekuwa wakitafuta mbuzi wa kumtoa kafara, ili upepo upite. Pep Guadiola pia aliwatupia lawama, madaktari wa klabu yake ya Bayern Munich baada tu ya kula kichapo cha goli 3-1 mbele ya FC Porto ya Ureno katika michuano ya klabu bingwa ulaya mwaka jana.

Je, hali itakuwaje Stamford Bridge? Tusubiri kuona nini kitajiri siku za usoni. Je, utawala wa juu utayabariki maamuzi ya Mourinho dhidi ya daktari huyo? Na vipi timu, itapata matokeo mfululizo baada ya kuondolewa kwa daktari huyo katika benchi? Muda utasema.

VIDEO:MOURINHO NA EVA CARNEIRO WAKIRUSHIANA MANENO BAADA YA KUINGIA UWANJANI KWENDA KUMTIBU HAZARD


WANASOKA WATATU WENYE FOLLOWERS WENGI INSTAGRAM HAWA HAPA....

$
0
0
Mtandao wa Instagram ni maarufu sana hivi sasa. karibia kila mtu maarufu anatumia mtandao huu. 
Hivi karibuni mtandao wa cosmopolitan.com ulitoa orodha ya watu maarufu wenye followers(wafuasi) wengi kwenye Instagram.
Kwenye hiyo orodha  mwanamuziki Beyonce anaongoza kwa kuwa na wafuasi milioni 42.7. 
Lakini kwa upande wa soka namba moja ni Neymar ambaye ana likes Milioni 29.4. Kwenye list ya dunia Neymar yupo namba 10.
Namba mbili kwa upande wa wanasoka ni Cristiano Ronaldo ana wafuasi Milioni 26.1, kwa upande wa dunia yupo nafasi 13.
Namba tatu kwa upande wa wanasoka ni Leo Messi ana wafuasi Millioni 22.3 na kwa dunia yupo namba 18.

DE GEA HACHEZI TENA MECHI IJAYO DHIDI YA ASTON VILLA – VAN GAAL

$
0
0
Kipa ambaye  anatakiwa kwa hamu kubwa na Real Madrid bado ataendelea kukaa benchi kwenye mechi ijayo dhidi ya Aston Villa kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa ufunguzi.
Licha ya De Gea kusema kwamba yupo tayari kucheza kwa sasa, lakini kocha wake, Louis Van Gaal amesema kwamba hatacheza kwenye mechi ijayo. 
De Gea atakosa hiyo safari kwasababu bado yupo kwenye hali ile ile iliyosababisha kukosa namba mechi ya kwanza ambayo ni kutokuwa sawa kisaikolojia.
De Gea anahusishwa sana na kuhama klabu ya Manchester United na Kwasababu kipindi cha usajili bado kipo, basi kipa huyo yupo kwenye tatizo hilo.

ZIDANE AJA NA LAKE HUKO REAL MADRID..

$
0
0

Gwiji wa zamani wa Real Madrid na Ufaransa, Zinedine Zidane amempa mwanaye Enzo unahodha wa kikosi cha pili cha Real Madrid.


Zidane ndiyo kocha wa timu B ya Madrid maarufu kama Castilla, na ameamua kumpa mwanaye huyo.

Ingawa inaonekana ni kama zengwe kwa kuwa Enzo alicheza soka katika kikosi cha daraja la kwanza inayojulikana kama Tercera, kabla ya kujiunga na Madrid B aliyopandishwa.

Hana muda wa kutosha kiasi cha kupewa unahodha wa kikosi B kwa kuwa alicheza daraja la tatu yaani Segunda B kabla ya kutua kikosi B.


Lakini Zidane amefunga masikio na kumwamini mwanaye huyo ambaye amempa unahodha.

MZUNGU WA SIMBA NA MAGURI MAMBO YACHACHA....

$
0
0
Ingawa suala limekuwa likienda kwa siri kubwa lakini ukweli ni kwamba Kocha Dylan Kerr wa Simba ameishaeleza kutoridhishwa na kiwango cha Elius Maguri na yuko tayari aachwe.

Habari za ndani kutoka ndani ya Simba zimeeleza kocha huyo Mwingereza ameonyesha kutovutiwa na kiwango cha Maguri, hivyo ameuambia uongozi unaweza kumuonyesha mlango wa kutokea.

"Ni kweli, kocha ndiye amesema kwamba haridhishwi na Maguri. Amefanya naye kazi kwa zaidi ya mwezi sasa na anaona hafurahishwi naye.


"Kuhusiana na kumuacha kwenye kikosi ilikuwa ni siku ya Simba Day, lakini unaona Maguri kwa nini hakutambulishwa. Ilitakiwa atambulishwe kama wachezaji wengine, lakini akatolewa kabisa.

"Hapo utapata jibu kwamba Maguri hana chake Simba ingawa inaonekana anakosekana wa kumueleza ukweli," kilieleza chanzo.
Lakini jana mchana, Rais wa Simba, Evans Aveva amesema suala hilo limerudishwa kwenye kamati ya usajili.
"Kocha ndiye alitaka Maguri aondolewe kwenye kikosi siku ya Simba Day. Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wadau kwamba tunawaingilia makocha, hasa klabu hizi kubwa za Simba na Yanga.
"Sisi hatukutaka hilo litokee, tukampisha kocha afanye kazi yake," alisema Aveva.
"Lakini suala la Maguri liko kwenye kamati ya usajili, mnajua huyo ni mchezaji wetu kabisa," alisema Aveva.

Via Salehehjembe

USIPITWE NA ISHU HII YA IVO MAPUNDA NA SIMBA......

$
0
0
Golikipa mkongwe nchini,  Ivo Philip Mapunda amesema yuko tayari kusaini mkataba na klabu yake ya Simba, lakini amekuwa haelewi kama kweli wekundu hao wa Msimbazi wanamhitaji tena.
Ivo amekaririwa na  Salehjembeakisema kamwe hajakimbia kama ambavyo imekuwa ikielezwa.
“Nimekimbia vipi, mara ya mwisho niliondoka kambini Lushoto baada ya kuumia. Collins (Kaimu Katibu Mkuu) alinieleza atanipa mkataba.
“Nimekuwa nikisubiri na hata niliwasiliana na kocha pamoja na Collins, bado inaonekana kuna sintofahamu.
“Si kweli nimekimbia, nipo tayari lakini vizuri nao wakaonyesha wana nia kweli ya kufanya kazi na mimi,” alisema Ivo.
Kuhusiana na hilo, Rais wa Simba, Evans Aveva amesema wanachosubiri na Ivo ni kusaini mkataba tu.
“Kuhusu Ivo tulishamalizana, tunachosubiri kusaini naye mkataba. Hatukumpata kumalizana naye lakini taarifa zinaeleza yuko jijini Dar.
“Hivyo itakuwa lahisi kumpata na  kumalizana naye. Baada ya kusaini mkataba, basi tutawapa taarifa,” alisema Aveva.

Ivo aliumia wakati akiwa Lushoto akalazimika kuondoka kambini kwenye kupata matibabu. Makubaliano yake na Simba ni kuongeza mkataba wa mwaka mmoja, jambo ambalo linaelezwa litafanyika kati ya leo, kesho na keshokutwa.
Viewing all 1447 articles
Browse latest View live