Quantcast
Channel: MPENJA SPORTS
Viewing all 1447 articles
Browse latest View live

BAYERN ILIYOJERUHIWA YAIRARUA VIBAYA JUVE NA KUITUPA NJE UEFA

$
0
0
Bayern Munich imepambana kutoka nyuma kwa goli 2-0 hadi kuichapa Juventus kwenye dakika za nyongeza na kusonga mbele kwenye hatua ya robo fainali ya Champions League.
Timu hizo zilitoka sare ya kufunga kwa bao 2-2 kwenye mchezo wa kwanza, Paul Pogba na Juan Cuadrado wakaifungia Juve na kuiweka mbele kwa bao 2-0 dhidi ya Bayern kwenye mchezo wa jana usiku.
Robert Lewandowski alipiga bao kwa kichwa na kufufua matumaini ya Bayern kubadili matokeo kabla ya Juve kumruhusu Thomas Muller kusawazisha katika dakika ya mwisho na kuufanya mchezo kuwa sare ya magoli 2-2 na kulazimisha timu hizo kwenda kwenye dakika za nyongeza.
Bayern wakafuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya kwa style ya aina yake baada ya Thiago na Kingsley Coman kuifungia timu yao mabao mawili katika muda wa nyongeza. Mchezo huo ukamalizika kwa Bayern kuichapa Juve magoli 4-2 na kufanya jumla ya magoli yote ya michezo miwili kuwa Bayern 6-4 Juve.
Juve ambao walitawala mchezo kwa asilimia nyingi za muda wa kawaida walichanganywa na goli la kusawazisha la dakika za lala salama la Muller pamoja na mabadiliko yaliyofanywa na Guardiola ya kuwaingiza Coman na Thiago ambao waliamua mchezo.
Mbali na kupoteza mchezo huo, kinachowaumiza zaidi Juve ni goli lilifungwa na Coman mchezaji wao kinda ambaye yupo Bayern kwa mkopo wa muda mrefu.
Kijana huyo wa kifaransa mwenye miaka 19, ali-assist magoli matatu wakati Bayern inashinda bao 5-0 dhidi ya Werder Bremen kwenye mchezo wao wa ligi weekend iliyopita na alikuwa kwenye kiwango bora baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Xabi Alonso.

Baada ya Messi kupachika goli dhidi ya Arsenal jana, hawa ndio wafungaji wa Barcelona wanaoongoza kwa magoli mengi UEFA

$
0
0
Leo Messi 83
Rivaldo Ferreira 22
Patrick Kluivert 20
Luis Enrique 19
Neymar 17

KEANE ARUSHA RUNGU KWA WENGER BAADA YA KIPIGO CHA AIBU KWA BARCELONA

$
0
0
Former Manchester United captain Roy Keane has launched a scathing attack on Arsenal's players  
Roy Keane amedai kwamba Arsene Wenger ana kundi kubwa la wachezaji ambao wengi wao ni dhaifu na kuwashutumu wachezaji wa Arsenal kuwadanganya mashabiki wao.
Arsenal jana walitupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Barcelona katika dimba la Camp Nou.
Vile vile wametupwa nje ya michuano ya FA baada ya kufungwa na Watford Jumapili iliyopita huku wakikabiliwa na shughuli pevu ya kupunguza pengo la alama 11 dhidi ya vinara Leicester ambao wanapewa nafasi kubwa ya kutwaa ndoo msimu huu.
“Hii inadhihirisha kuwa wana wachezaji wengi ambao ni dhaifu ambao kwenye baadhi ya michezo yenye uzito hawana msaada wowote,” nahodha huyo wa zamani wa Man United aliiambia ITV.
“Hakuna shaka kwamba presha ya mashabiki kwa miezi ya hivi karibuni imewayumbisha sana, sasa kama huwezi kustahimili presha ya mashabiki basi haupaswi kuwa pale", aliongeza
“Inavyoonekana dhahma ilikuwa tayari ilishafanyika kwenye mchezo wa awali. Sidhani kama kuna aibu kubwa baada ya kupoteza kwa idadi ya magoli 3-1 juhudi zimeonekana - lakini nadhani Barcelona walijua jinsi gani ya kuwadhibiti", alimalizia.

LUIS ENRIQUE AMEJIBU HAIVI BAADA YA KUULIZWA NI TIMU GANI ANAIOGOPA ULIMWENGUNI

$
0
0
Luis Enrique fears nobody in Champions League draw
Kocha wa Barcelona Luis Enrique amesema kwamba,kama kuna timu ambayo angeihofia sana katika Ligi ya Mabingwa Ulaya basi ni Barcelona.
Enrique jana alishuhudia timu yake ikiitupa Arsenal nje ya michuano hiyo kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na Messi, Neymar na Suarez huku katika mchezo wa kwanza uliopigwa katika dimba la Emirates wakishinda magoli 2-0. 
Kwa sasa Barca itapambana na timu kati ya Bayern Munich, Atletico Madrid, Real Madrid, Paris Saint-Germain, Manchester City, Wolfsburg na Benfica baada ya kufanyika kwa droo itakayochezeshwa kesho Ijumaa.
Bareclona wako katika moto usiopimika baada ya kutopoteza mchezo wowote katika mechi 38 mpaka sasa.
"Timu pekee ambayo nisingependa kukutana nayo ni Barca," Luis Enrique alisema.
"Ni dhahiri kwamba tuna wachezaji wa kipekee, lakini mwishi wa siku kitu kizuri zaidi ni kwamba wachezaji wanacheza kwa ushirikiano mkubwa katika nyakati zote za kushambulia na kulinda.
"Tuna furaha kubwa kwamba Messi, Suarez na Neymar ni washambuliaji wetu .

NEY WA MITEGO, ROMA MKATOLIKI WALIA NA WENGER

$
0
0
Baada ya jana usiku Arsenal kukubali kipigo cha bao tatu moja kutoka kwa Barcelona wasanii hawa kwa nyakati tofauti walionyesha hisia zao za maumivu na kutupa lawama za moja kwa moja kwa kocha wa klabu hiyo mzee Wenger.
Kwa upande wake Nay wa mitego alikuwa na haya ya kusema "Acha tu tukalale maana hawa Arsenal watakuja kututia uchizi. Huyu mzee Wenger angekua Tanzania ningeshamchana pumbafu.! Dj White kaka usinipigie simu niache nikapumzike, wewe Kabuka naku block ukiendelea na kelele zako".
Kwa upande wake Roma Mkatoliki alipost picha ikimuonyesha akiwa mtu mwenye masikitiko huku akitizama mechi iliyokuwa ikichezwa jana usiku na kuandika kuwa hakuna kitu au mtu anaye mnyima raha kama Wenger.
Lakini mbali na hawa mashabiki wengi wa Arsenal wamekuwa wakilalamika na malalamiko yao yapo moja kwa moja kwa kocha huyo.
Credit:EATV

MAMBO MANNE YA KUANGALIA NI KWA NINI ARSENAL ILIKUWA NI LAZIMA WATOLEWE

$
0
0
Arsenal waliingia katika mchezo wa jana wakiwa ama hawana nafasi kabisa au wana nafasi finyu ya kufuzu robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hapa chini ni baadhi ya mambo ambayo yameonekana katika mchezo wa jana;

Vikosi vya timu zote mbili 
Kwa kuanzia na Barcelona ambao ndiyo walikuwa wenyeji wa mchezo huo, kulikuwa na mabadiliko ya mtu mmoja tu ukilinganisha na kikosi kilichoanza dhidi ya Arsenal katika raundi ya kwanza, Jeremy Mathieu alianza akichukua nafasi ya Gerald Pique aliyekuwa na kadi mbili za njano. Utatu mtakatifu unaoundwa na Luis Suarez, Neymar na Lionel Messi kama ilivyoada ilikuwa ni kupeleka kilio kwa washika bunduki wa London.

Kwa upande mwingine, Arsenal ambao alikuwa wageni katika mchezo huo, walifanya mabadiliko ya wachezaji sita katika kikosi chao ukilunganisha na kile kilichoanza wiki mbili zilizopita.
Lakini 'talking point' hapa ni Alex Iwobi  na Flamini ambaye wamemtunga jina la  “master of ceremony” wa mchezo wa kwanza baada ya kunogesha ushindi wa Barcelona kutokana na kumfanyia madhambi ndani ya eneo la 18 punde tu baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Francis Coquelin.
Iwobi ambaye ni kinda wa Kinigeria alikuwa akicheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya timu bora ulimwenguni. Alikuwa akipambana kwenye eneo la kiungo na wachezaji kama Iniesta, Rakitic na Busquests ambapo katika hali ya ni jambo lisiloweza kuelezeka kwamba inawezekanaje Iwobi kupambana na nyota hao kutokana na namna walivyo na uwezo mkubwa.

Mbinu za kiufundi
Wakicheza kwa kujiamini na kutumia  mfumo uliozoeleka tangu enzi za kocha wao wa zamani Pep Guardiola, Barcelona walikuwa hawana presha kubwa kutokana na kuwa na hazina ya mabao mawili waliyopata katika dimba la Emirates wiki mbili zilizopita. 
Arsenal wana tabia ya kucheza mpira wa aina moja na Barcelona lakini uwezo wao mdogo wa mchezaji mmoja mmoja huku wakati huo huo wakidaiwa magoli mawili kuliwafanya wapoteze kujiamini na kukosa mwamko wa kuitoa Barca. 
Wakati Barcelona wana wachezaji wenye uwezo wa kubadili matokeo muda wowote, wao Arsenal wachezaji wao wengi wao ni 'tia maji tia maji'
Arsene Wenger alisema kuwa wao walienda pale kwa dhumuni la kushambulia tu ili kufanya yasiyowezekana kuwezekana. Kwa kufanya hivyo akaamua kuwaanzisha wachezaji wenye kasi kama vile Danny Welbeck, Alex Iwobi na El Neny ili kufanya mashambulizi ya kushtukiza japo hawakufanikiwa kutokana na watatu hao kukosa umakini golini. 
Kuanzia katika eneo la kiungo mpaka safu kali kabisa ya ushambuliaji, Barcelona ina wachezaji ambao muda wowote wanaweza kubadilisha matokeo ya mchezo, kwa mafano ' Katika mchezo wa jana, makosa madogo yaliyofanywa na mabeki wa Arsenal yalitosha kumpa Messi nafasi ya kuwaangamiza Arsenal.

Arsenal kwa namna nyingine imekuwa ni timu inayomtegemea maajabu ya Ozil na akibanwa tu basi kila kitu kinashindikana. 
Mchezaji bora wa Arsenal msimu uliopita Alexis Sanchez amekuwa hayuko katika kiwango bora msimu huu na katika mchezo wa jana amefanya 'slides' na 'slips' nyingi kuliko mashuti yaliyolenga langoni.
Ozil naye ni mchezaji ambaye amekuwa aking'ara pale timu inapokuwa iki-possess mpira na ndipo ambapo mara nyingi madhara yake huonekana, lakini pale timu inapokuwa imeelewa kamwe hutamwona kama Ozil ni mchezaji mzuri.

Kukosekana kwa 'consistency' katika timu.
Tatizo kubwa la Arsenal kwa miaka mingi limekuwa ni kukosekana kwa 'consistency' hasa wanapotakiwa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya timu. Pengine hali hii inatokana na uwepo wa wachezaji kutoka katika akademi ya klabu hiyo ambao mara nyingi wanaamini katika kupiga pasi nyingi ili wapandishwe timu ya wakubwa. 
Wanakosa matamanio ya kuwa mabingwa tofauti na inavyoonekana kwa wachezaji wa timu nyingine.
Mtazamo wa wachezaji wa Arsenal lazima ubadilike ili waweze kuendana na ushindani uliopo sasa. Hiyo ndiyo itawarudisha katika enzi za 'invisibles'.
Suala la mwisho ni kwamba, katika mchezo wa jana Barcelona waliitawala Arsenal kwenye kila idara, lakini vile vile Arsene Wenger bado ni kocha mzuri ila kuna mambo anayotakiwa kukubali kubadilika, hasa katika suala la ununuzi wa wachezaji wenye majina makubwa na wenye uwezo mkubwa wa kubadilisha matokeo uwanjani pindi timu inapohitaji kufanya hivyo.

VIINGILIO YANGA DHIDI YA APR VYA HADHARANI

$
0
0
Kwa ujumla eneo lote la mzunguko linalohusisha viti vya rangi ya Chungwa, Kijani na Bluu watu wataketi kwa Sh. 5,000.
VIP A tiketi yake itanunuliwa kwa Sh. 25,000, wakati VIP B na C kote kila tiketi itauzwa Sh. 20,000.
Tiketi zitaanza kuuzwa mapema siku ya mchezo, Jumamosi katika maeneo ya siku zote, ikiwemo Uwanja wa karume na Uwanja wa Taifa.

JUMA ABDUL KUWAKOSA APR JUMAMOSI

$
0
0
Yanga itacheza bila beki wake wa kulia, Juma Abdul katika mechi yake dhidi ya APR katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika keshokutwa Jumamosi.
Juma Abdul ana kadi mbili za njano na tayari Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limeitaarifu Yanga kukumbuka hilo.
Beki huyo ndiye aliyefunga bao la kwanza wakati Yanga ikiitwanga APR kwa mabao 2-1 kwao Kigali.
Lakini katika mechi hiyo, akapigwa kadi ya njano na kufanya saa akose mchezo huo.

WANNE HAWA WA YANGA KUIKOSA APR JUMAMOSI

$
0
0
Wachezaji wanne wa Yanga wataendelea kubaki jukwaani wakati Yanga ikipambana na APR ya Rwanda katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika keshokutwa Jumamosi.
Said Juma ‘Makapu’ ana maralia, Simon Matheo ni majeruhi, nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’ bado majeruhi. Huku Juma Abdul akiwa na kadi mbili za njano.
Yanga in a kibarua kigumu dhidi ya APR licha ya kwamba ilianza kwa ushindi wa mabao 2-1 ugenini.
Juma Abdul ana kadi mbili za njano na tayari Shirikisho la Soka Afrika (Caf), limeitaarifu Yanga kukumbuka hilo.
Credit:Salehjembe

VIDEO: LIVERPOOL YAITUPA NJE MAN UNITED EUROPA, MATOKEO YA MECHI NYINGINE YAKO HAPA

$
0
0
Bao la Manchester United lilifungwa na Martial dakika ya 32.

Michuano ya Europa League imeendelea tena usiku wa kuamkia leo kwa michezo nane ambapo Liverpool wametinga robo fainali baada ya kutoka sare ya 1-1 na wenyeji, Manchester United katika Uwanja wa Old Trafford.
Manchester United walianza kuandika bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na Anthony Martial dakika ya 32 kipindi cha kwanza ambao ulijaa wavuni.
Liverpool ikasawazisha bao hilo kupitia kwa Philippe Coutinho katika dakika ya 45 kipindi cha pili.
Hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika matokeo ikawa ni sare ya bao 1-1, lakini Liverpool ikisonga mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-1 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 ilioupata katika mchezo wa awali wakiwa ugenini.
Na katika matokeo mengine Tottenham nayo imeaga michuano hiyo baada ya kufungwa 2-1 na Borussia Dortmund, Mabao yote ya Dortmund yamefungwa na mwanasoka bora wa Afrika, Pierre-Emerick Aubameyang dakika ya 24 na 70, wakati bao la Spurs limefungwa na Heung-Min Son dakika ya 73.
Dortmund inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 5-1, baada ya wiki iliyopita kushinda 3-0 Ujerumani.
Sevilla imeifunga 3-0 FC Basel, mabao ya Adil Rami na Kevin Gameiro mawili Uwanja wa Ramon-Sanchez Pizjuan, hivyo kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-0 baada ya awali kutoa sare ya 0-0 ugenini.
Shakhtar Donetsk imeshinda ugenini 1-0 dhidi ya RSC Anderlecht, bao pekee la Eduardo Alves da Silva dakika za majeruhi Uwanja wa Constant Vanden Stockstadion, hivyo inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 4-1 baada ya awali kushinda 3-0 nyumbani.
Video ya magoli Man United vs Liverpool

KUMBE GOLI LA COUTINHO JANA DHIDI YA MAN UNITED ALILIFANYIA MAZOEZI MIAKA MINNE NYUMA!!! (VIDEO)

$
0
0
Inawezekana Guillermo Varela alishawahi kuangalia video ya goli la Philippe Coutinho akiwa kwenye mazoezi wakati akiwa Inter Milan?
Beki huyo wa kulia wa Manchester United alifungashwa na Coutinho sekunde chache kabla ya half-time kisha m-brazil huyo akafunga bao la aina yake kwenye mechi ya ugenini katika uwanja wa Old Trafford.
Varela hakudhani kama Coutinho angeweza kufunga goli hilo kutokana na sehemu aliokuwepo, lakini huku akiwa anatoka nje ya uwanja, m-brazil huyo aliu-chip mpira uliompita David De Gea asijue nini cha kufanya.
Muda mfupi baada ya kufungwa kwa goli hilo, ikaonekana video ya goli jingine la Philippe Coutinho alilofunga kwenye mazoezi wakati akiwa Inter Milan linalofanana kwa kila kitu na goli alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Man United.

Angalia goli alilofunga Philippe Coutinho akiwa Inter Milan linalofanana na lile alilofunga kwenye mechi dhidi ya Manchester United


DORTMUND, LIVERPOOL WACHONGANISHWA EUROPA LEAGUE...RATIBA NZIMA HII HAPA...

$
0
0
Hii ndio ratiba ya Europa ligi iliyotolewa leo na Shirikisho la soka barani Ulaya, Uefa.

RATIBA YA ROBO FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE YATOKA.....

$
0
0
Ratiba ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya imetolewa leo ambapo mabingwa watetezi, FC Barcelona wamepangiwa na miamba mingine ya ligi ya Hispania, La liga, Atletico Madrid, huku mabingwa mara nyingi zaidi wa kihistoria, Real Madrid ambao wameshinda mataji 10 wakikabidhiwa Wolfsburg ya Ujerumani.
Angalia picha juu kujua mechi zote za robo fainali.

TFF YAZITUMIA SALAMU YANGA, AZAM FC

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limezitakia kila la kheri vilabu wawakilishi wa Tanzania kwenye michuano ya kimataifa, timu za Azam FC na Yanga SC katika michezo yao watakayocheza wikiendi hii.
Katika salamu hizo, TFF imezitakia kila la kheri timu hizo kuhakikisha zinafanya vizuri katika michezo yao ili ziweze kusonga mbele katika hatua inayofuata, na kuwapa furaha washabiki wa mpira wa miguu pamoja na watanzania wote.
Kesho Jumamosi, Yanga SC watakuwa wenyeji wa APR ya Rwanda katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa (CAF CL) kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, mchezo utakaochezeshwa na mwamuzi Bernard Camille, akisaidiwa na Eldrick Adelai, Gerard Pool na Allister Bara kutoka nchini Shelisheli.
Jumapili Azam FC watakua wakicheza dhidi ya Bidvest FC kutoka nchini Afrika Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho (CAF CC) kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi, mwamuzi wa mchezo huo ni Gait Oting akisaidiwa na Abdallah Gassim, Casim Dehiya, mwamuzi wa akiba Ariel James wote kutoka Sudan Kusini

WATANZANIA WAPATA SHAVU CAF.....

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu barani Afrika (CAF) limetoa orodha ya waamuzi watakaochezesha na kusimamia michezo ya Kombe la Shirikisho Afrika (CC), kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) pamoja na kuwania kufuzu kwa Fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) mwaka 2017.
Michael Richard Wambura ameteuliwa kuwa Kamisaa wa Mchezo Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) kati ya Al Shandy ya Sudan dhidi ya FC Lupopo mchezo utakaochezwa siku ya Jumapili nchini Sudan.
Mwamuzi Israel Mujuni akisaidiwa Frank Komba na Soud Lila, mwamuzi wa akiba akiwa ni Mfaume Ali Nassoro katika mchezo kati ya Renaissance Football Club (Chad) v E.S.T. (Tunisia) wa Kombe la Shirikisho Afrika (CAF CC) nchini Chad.
Mchezo namba 97 wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika (AFCON) kati ya Lesotho v Shelisheli Machi 29, 2016 utachezeshwa na Israel Mujuni akisaidiwa na Ferdinand Chacha, Samuel Mpenzu huku mwamuzi wa akiba akiwa Waziri Sheha.
Mwamuzi Mfaume Ali Nassoro atachezesha mchezo kati ya Burundi v Congo DR kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20), Aprili 4, 2016 mjini Bunjumbura akisaidiwa na Frank John Komba, Alli Kinduli, huku Martin Eliphas Saanya akiwa mwamuzi wa akiba.

TWIGA STARS KUWAFUATA ZIMBABWE LEO

$
0
0
Msafara wa watu 25 wa timu ya Taifa ya Wanawake ya mpira wa miguu “Twiga Stars” unatarajiwa kuondoka leo majira ya saa 4 usiku kuelekea nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa marudiano kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake utakaochezwa siku ya Jumapili mjini Harare.
Twiga Stars inayonolewa na kocha mkuu, Nasra Juma inaondoka ikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mchezo huo wa marudiano, baaada ya kuwa kambini kwa takribani wiki mbili kwa maandalizi ya mchezo huo.
Nasra amesema makosa yaliyojitokeza katika mchezo uliopita nyumbani, wameyafanyia kazi na sasa wana imani ya kufanya vizuri siku ya Jumapili katika uwanja wa Rufaro mjini Harare na kuweza kusonga mbele katika hatua ya pili.
Mkuu wa msafara ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji na Mwenyekiti wa Kamati ya Soka la Wanawake TFF, Amina Karuma, benchi la ufundi litaongozwa na kocha mkuu Nasra Juma, kocha msaidizie Elyutery Muholery, kocha msaidizi Edina Lema, daktari wa timu Anange Lwila, mtunza vifaa Esther Chaburuma na meneja wa timu Furaha Francis.
Wachezaji wanaosafiri leo ni Fatuma Omary, Stumai Abdallah, Maimuna Khamis, Fatuma Issa, Anastazia Katunzi, Donisia Minja, Happyness Mwaipaja, Wema Richard na Amina Bilal.
Wengine ni Asha Rashid, Mwanahamis Omary, Belina Julius, Fatuma Bashiri, Fatuma Khatibu, Mwajuma Abdallah, Amina Ramadhani, Fatuma Mustafapha na Neema Kiniga.

WASHAMBULIAJI WATANO RAIA WA AMERIKA KUSINI WANAOONGOZA KUTIKISA NYAVU EPL HAWA HAPA

$
0
0
Mchezo wa soka umekuwa ni kama utamaduni na kazi kwa nchini nyingi za Amerika ya kusini hasa Brazil, Argentina, Uruguay, Chile, Peru, Mexico, Paraguay na nyingine nyingi.
Amerika ya kusini imewahi kutoa wachezaji wenye majina makubwa kama vile Pele, Maradona, Ronaldo, Messi ambaye bado ni mwiba kwa sasa.
Katika maeneo mbalimbali kama shuleni, mitaani, viwanja vidogo vidogo na kwenye fukwe huko Amerika ya Kusini utawakuta watu wakikusanyika na kushindana kuonesha ujuzi wao wa kuuchezea mpira.
Kwa mafano kwenye mitaa mbalimbali ya jiji la Rio de Janeiro huko Brazil, utawaona vijana wakishindana kucheza soka peku peku kuanzia asubuhi kunapokucha mpaka jua linapozama katika viwanja ambavyo havina ubora huku vile vile mipira wanayochezea ikikosa ubora.
Kwa kufanya hivyo, hali hii hupelekea kuwa na viwango vikubwa na baadye kusajiliwa na timu kubwa ulimwenguni na kuwa wachezaji wenye majina makubwa duniani hasa sehemu za Ulaya ambapo mpira unalipa kupindukia.
Ligi Kuu nchini England imekuwa ikipokea wachezaji wengi kutoka Amerika ya Kusini hasa washambuliaji. Wengi wao wamekuwa wakicheza kwa mafanikio kutokana na uwezo wao mkubwa wa ama kuwasumbua mabeki au kupachika mabao .
Sasa hapa tunawatupia jicho washambuliaji 5 kutoka Amerika ya Kusini ambao wamewahi kuwa vinara wa mabao EPL.

5. Nolberto Solano – magoli 49 
Solano alikuwa ni mchezaji wa kwanza kutoka Peru kucheza kunako Ligi Kuu ya England baada ya kusajiliwa na Newcastle United mwaka 1998 akitokea klabu ya Boca Juniors. Alicheza klabuni hapo kwa vipindi viwili na kufunga mabao 37 katika michezo 240.
Kiungo huyo wa zamani wa Peru pia alicheza Aston Villa ambapo alicheza michezo 48, akifunga mabao 8 na vile vile West Ham United mwaka 2007-08 na kufunga mabao 4 katika michezo 23.

4. Gus Poyet – magoli 54
Poyet alielekea Premier League mwaka 1997 akitokea kunako klabu ya La Liga ya Real Zaragoza akijiunga na Chelsea ambapo alifanikiwa kufunga mabao 36 ndani ya michezo 105.
Meneja huyo wa zamani wa Sunderland, badaye alihamia Tottenham mwaka 2001 na kufunga mabao 18 katika michezo 82 kabla ya kuamua kutundiga daluga.

3. Luis Suarez– magoli 69
Huyu alidumu katika klabu ya Liverpool kwa misimu minne na kufunga mabao 69.
Alijiunga na Liverpool mwaka 2010 akitokea kunako klabu ya  Ajax ya Uholanzi. Alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka mara moja, tuzo ya PFA ya mwaka na kutwaa tuzo ya mfungaji bora wa Ulaya mwaka 2014.

Ni mchezaji pekee katika hostoria ya EPL kufunga 'hat-tricks' tatu dhidi ya klabu moja aambayo ni Norwich City.

2. Carlos Tevez – magoli 84
Tevez ni moja ya wachezaji wachache kuweza kucheza klabu mbili za jiji la Manchester kwa nyakati mbili tofauti na kufanikiwa kufunga mabao 84 katika EPL.
Alifunga mabao 7 kwenye michezo 26 wakati akicheza West Ham United kabla ya kujiunga na Manchester United na kufunga mabao 19 kwenye michezo 63.
Baadaye mwaka 2009, Tevez alihamia klabu ya Manchester City na kufunga mabao 58 kwenye michezo 113 kwa misimu minne aliyodumu klabuni hapo.

1. Sergio Aguero – magoli 94
Sergio Aguero, ambaye kwa sasa ni moja ya washambuliaji bora duniani, alimzidi Muargentina mwenzake Novemba 2015 alipofunga goli dhidi ya Liverpool katika dimba la Etihad.
Mshambulizi huyu wa zamani wa Atletico Madrid anaweza kufunga magoli zaidi endapo tu ataamua kuendelea kubaki Ligi Kuu England.
Aguero kwa sasa ameshadumu klabuni hapo kwa misimu minne.
Alijiunga na Man City mwaka 2011 akitokea klabu ya Atletico Madrid.

RATIBA YA MECHI ZA LEO LIGI KUU ENGLAND HII HAPA

NEYMAR NAYE AINGIA KWENYE MTEGO WA UKWEPAJI KODI UHISPANIA

$
0
0
Nyota wa Barcelona Neymar, anashutumiwa kwa kuficha baadhi ya taarifa za mapato yake kuanzia alipokuwa Santos, Barcelona (mpaka sasa) na mikataba yake ya Nike. Mapato hayo yanakadiriwa kufika kiasi cha Yuro milioni 45.9. Vielelezo vya mahakama vinaonyesha kwamba Neymar alitumia makampuni yake (Neymar Sport e Marketing, N & N Consultoria, N & N Administracao de Bens) kukwepa kulipa Yuro mil 56.4 kati ya mwaka 2012 na mwaka 2014.
Jaji alitoa shutuma hizo na kusema kuwa Neymar alikuwa na mikataba feki ili kuficha vyanzo vyake vingine vya mapato. "Tuliangalia kwa makini taarifa kuhusu masuala ya kodi juu ya Neymar, biashara zake tatu na washirika wake katika biashara (wazazi wake) na tulijiridhisha kukuta udanganyifu katika biashara hizo", aliandika Develly Claudia Montez ambaye alikuwa mkaguzi wa mahakama.
Kwa sasa Neymar yuko kwenye shihikizo kubwa la uchunguzi wa tuhuma za ukwepaji kodi dhidi ya serikali ya Uhispania. Huyu si mchezaji wa kwanza wa Barcelona kukumbana na tuhuma kama hizi, kwani nyota mwingine wa klabu hiyo Lionel Messi na Javier Mascherano pia waliingia katika mtego huo.

EVERTON VS ARSENAL: MAMBO MUHIMU YA KUZUNGATIA KUELEKEA MCHEZO HUU

$
0
0
Giroud ana rekodi nzuri mbele ya Everton

Leo kunako majira ya saa tisa na dakika 45 katika dimba la Goodson Park miamba miwili ya Everton na Washika Bunduki wa London Arsenal watatupa karata zao kupigania pointi tatu muhimu.
Kuelekea katika mchezo huu, timu zote mbili zinaingia uwanjani zikiwa na kumbukumbu tofauti kwa michezo yao iliyopita. Everton wanaingia wakiwa na kumbukumbu ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chelsea katika kombe la FA na kutinga hatua ya nusu fainali
Arsenal kwa upande wao, wanaingia uwanjani wakiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Barcelona katika michuano ya UEFA walichokipata katikati mwa wiki iliyopita, vile vile kipigo dhidi ya Watford cha mabao 2-0 katika dimba la Emitares na kutupwa nje ya michuano ya FA.
Hivyo basi, huu ni mchezo unaookena kuwa mgumu kutokana na timu zote mbili kuwa na ari tofauti, Everton wakihitaji kuendeleza ushindi dhidi ya vigogo hatimaye kupanda nafasi za juu mwa msimamo wa ligi na walau kupata nafasi ya kushiriki michuano ya EUROPA, ukizingatia nafasi ya 12 waliyopo kwa sasa.
Arsenal wanaingia wakiwa na malengo mawili tofauti, kwanza ni kufuta kumbukumbu ya matokeo mabovu mfululizo iliyopata katika michezo ya hivi karibuni dhidi ya Man United, Swansea, Barcelona, Tottenham na Watford. La pili ni kufufua matumaini yao ya kuwania ubingwa hasa ukizingatia kwa sasa wapo alama 11 nyuma ya vinara Leicester lakini wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Tukielekea moja kwa moja kwenye mchezo wenyewe, Everton wanaonekana kutokuwa na rekodi nzuri sana mbele ya Arsenal baada ya kuwa wameshinda mchezo mmoja kati ya 18 waliyokutana. Hivyo kuwa na kazi kubwa sana ya kuhakikisha ushindi unabaki Goodson Park.
Taarifa muhimu za vikosi vya timu zote mbili.
Winga wa kushoto wa Everton Bryan Oviedo amerudi baada ya kupona maradhi ya kifua ya liyokuwa yakimsumbua lakini anaweza asijumuishwe kikosini kutokana na kukosa utimamu wa mwili kuelekea mchezo wa leo. Kevin Mirallas na Gareth hawatokuwepo kutokana na kuendelea kutumikia adhabu zao.
Kwa upande wa Arsenal sasa, Mathieu Flamini hatakuwepo kwemye kikosi leo kutokana na kuuguza majeraha yake ya misuli ya paja aliyopata katika mchezo dhidi ya Barcelona katika mwa wiki kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa. Aaron Ramsey, Jack Wilshere, Petr Cech, Santi Cazorla na Alex Oxlade-Chamberlain wote wataendelea kukosekana kutokana na kuendelea kuuguza majeraha yao.

Mchezo utaanza majira ya saa 9.45 Alasiri katika dimba la Goodison Park.

Takwimu muhimu 

  • Everton wameshinda mchezo mmoja tu kati ya 18 ya mwisho 18 waliyokutana katika michuano yote (ameshinda mmoja, sare sita na kufungwa 11). 
  • Arsenal hawajashinda hata mchezo mmoja katika michezo yao mitatu ya mwisho waliyocheza katika dimba la la Goodson Park (sare 2 na kufungwa mmoja). 
  • Olivier Giroud amefunga magoli matano katika michezo yake mitano katika michuano yote dhidi ya Everton, ukijumuisha na michezo mitatu ya mwisho ya ligi dhidi ya wakali hao . 
  • Mesut Ozil amefunga magoli mawili na kutoa assists nne dhidi ya Toffees katika michuano yote. 
  • Everton wameshinda mchezo mmoja tu kati ya nane ya mwisho ya Ligi Kuu waliyocheza na Arsenal katika dimba la Goodison Park (wameshinda 1 droo 2 wamepoteza mitano). 
  • Arsenal wameshinda michezo yao miwili tu ya Premier League kati ya nane ya mwisho kuelekea mchezo huu wa leo (ushindi mara mbili, droo 4 na kufungwa mara tatu 3). 
  • Arsenal wamechukua alama 10 kati ya 27 ambayo wangetakiwa kupata (kushinda mara 2, droo nne, na kufungwa mitatu). 
  • Arsenal wamepiga mashuti macgache kabisa yaliyolenga lango wakiwa nje ya boksi msimu huu (25) na kufunga pia magoli machache kutokana na mashuti ya mbali (mawili dhidi ya Watford na moja dhidi ya Leicester). 
  • Everton wamecheza faulo chache kwenye Ligi Kuu kulinganisha na timu zote msimu huu (mara 235). 
  • Ni Arsenal tu ndiyo wanawazidi Everton kwa kupata kadi za njano msimu huu katika Ligi Kuu Uingereza. Arsenal wamepata kadi 33 huku Everton wakipata kadi 36.
    Viewing all 1447 articles
    Browse latest View live